Kuanazia leo lile tamko la Mkuu wa wilaya Bwana Makonda kuwa walimu katika wilaya Kinondoni wataweza kupanda mabasi bure kuanzia saa kumi na moja mpaka saa mbili na saa tisa mpaka kumi na moja jioni.Wengi wametoa maoni yao kuwa ni hatua nzuri katika kuboresha na kujali taaluma hii ambayo bado haina kipao mbele kikubwa katika nchi yetu licha ya kuwa ni nguzo muhimu katika maendeleo ya nchi yoyote duniani.Kwa miaka mingi kumekuwa na vilio juu ya maslahi yao ila mambo bado ni magumu sana.Tumaini langu kuwa kama huyu ameweza kuona hili itafika siku yataonwa na mengine lengo nikuweza kubadilisha hali ya walimu wetu.
Licha mtazamo huo wengine wamebeza na kusema hicho ni kitu kidogo sana kwani walimu wanayo matatizo zaidi ya hayo ni kweli na yanajulikana.Je tukiacha hayo nionavyo mimi inaweza ikawa changamoto mpya hasa kama kwa Makonda wa mabasi hao kuwa chanjo cha kuwatenga na kuwasema vibaya wale ambao tumezoea usafiri huu tunajua Makonda walivyo na maneno ya kashfa na jambo hili jema likwa shuburi licha la kupitishwa na wamiliki wao.Wito yapashwa elimu juu ya hili itolewe vizuri ili lisije likaeleweka vibay na kuwazalilisha walimu wetu wanaofanya kazi nzito na isihishie kuwa amri tu.Natumaini ipo siku walimu wataona faraja na kuthaminiwa zaidi.