Showing posts with label sports. Show all posts
Showing posts with label sports. Show all posts

Monday, February 8, 2016

Arsenal hawako tayari kiakili kushinda taji la Uingereza-Thiery Henry

Nguli wa Arsenal Thiery Henry anapata wasiwasi juu ya mwenendo wa timu yake ya zamani kama kweli ipo imara kifikra katika kugombea kombe la ligi kuu ya Uingereza.Mwenendo wa Arsenal umekuwa wa kususua na kupata matokeo yasiyo na uhakika.Hii inamsikitisha kwani anaona Leicester wana nguvu kifikra katika kutaka kuchukua kombe ila kwa Arsenal kuna walakini kidogo.Tuone katika mechi zijazo nini kitatokea.

Tokeo la picha la thierry henry arsenal pundit

Tuesday, January 26, 2016

JE WAJUA ADEBAYOR KALA SHAVU CRYSTAL PLACE

Emmanuel Adebayor raia wa Togo hatimaye amepata timu tena baada ya kukaa kwa kipindi kirefu maana ya kuachana na Tottenham.Sasa ni mali ya Crystal Palace.Hii ni baada ya Alan Pardew (Kocha)kudhibitisha hilo kuwa anamuhitaji Emma katika timu hiyo.

Emmanuel Adebayor

Sunday, January 24, 2016

ARSENAL KURUDI KILELENI LEO DHIDI YA CHELSEA

Asernal inaweza kurudi kileleni itakapo kutana na Chelsea kwenye dimba la Emirates.Arsenal ambayo inatabiriwa kuwa inaweza kubeba kombe msimu huu baada ya kulikosa kwa zaidi ya miaka 10.Mechi inatarajiwa kuanza saa moja kwa majira ya Afrika Mashariki.

kTokeo la picha la chelsea vs arseanl logoKikosi cha Arsenal-(P.Cech,P Mate,L KoScielny,N Monreal,H Berlin,M Ozil,A Ramsey,A Sanchez,M Flamini,J Campell,O Giroud

Chelsea:T Courtois,B Ivanovic,K Zouma,J Terry,C Azpilicueta,C Febregas,J Obi,P Rodriguez,N Matic,Willian,D Costa.

Sunday, January 17, 2016

ROONEY APIGA GOLI LA MWAKA AIPA MAN U POINTI TATU

Wayne Rooney licha ya kusakamwa na vyombo vya habari hivi karibu leo ameonyesha kile ambacho mashabiki wa Man U walikikosa siku nyingi baada ya kufunga goli maridadi katika dk 78' dhidi ya Liverpool na kuipa timu yake pointi tatu muhimu na kufikisha alama 37 huku ikishika nafasi ya tano katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.Liverpool licha ya kutengeneza nafasi nzuri za ushindi walishindwa kabisa kuweka mpira kimiani huku De Gea akiwa katika kiwango chake aliweza kuokoa nafasi nzuri za Liverpool kupata goli hivyo Liverpool inaendelea kuwa na pointi 31 ,nafasi ya 9 katika ligi kuu ya Uingereza.

Manchester United striker Wayne RooneyRooney akifunga goli nzuri dhidi ya Liverpool.

ARSENAL BADO BADO SANAAA UBINGWA UINGEREZA

Timu ya Arsenal imeshindwa kujikita kileleni mwa Barclays Premier ligi leo kwa kushindwa kupata pointi zote tatu muhimu katika kipindi hichi baada ya kuambulia sare tasa dhidi ya Stoke City.Kwa matokeo hayo Arsenal licha ya kuongoza ligi kwa tofauti ya magoli dhidi ya leicester City,kama wataendelea kucheza kwa kiwango cha leo basi Ubingwa wa Uingereza utaendelea kuwa historia tena.

Arsenal inakosa kiongozi imara ndani ya timu anayeweza kubadilisha matokeo ndio maana wanaishia kupiga pasi ambazo hazina manufaa na mwisho wanakosa matokeo hari ya wachezaji kutaka ubingwa kwa Arsenal iko mbali sana.Inabidi Wenger atambue vipindi ambavyo timu inahitaji ushindi kitu ambacho kimeo adibu sana kwa arsenal tangu kipindi kile cha kina Thiery Henry,Patrick Viera,Dennis Be,Wiltod,Fred L,Robert P n.k.timu inacheza mechi zote kwa kiwango kile kile.Kwa matokeo hayo Arsena mpaka sasa ina alama 44 nyuma ya Leicester alama 44 na Man City 44.

Arsenal Stoke

Thursday, January 14, 2016

Mohamed Elneny rasmi Arsenal Fc

Arsenal wamefanikiwa kumsajili kiungo mkabaji raia wa Misri Mohamed Elneny kwa ada ya uhamisho wa Pound 5m kutoka Balse ya Switzerland.Tayari tangu alhamisi ameanza mazoezi tayari kwa mechi za ligi kuu na championi ligi.Bado ndio kwanza ana umri wa miaka 23 hivyo atafanya makubwa kama ataweza kwenda na kasi ya ligi maarufu ya Barclays Premier Ligi.

Tokeo la picha la mohamed elneny

Wednesday, January 13, 2016

ARSENAL NA LIVERPOOL MTOTO HATUMWI DUKANI LEO USIKU CHELSEA MAN CITY WOTE UWANJANI,RATIBA YA MECHI NYINGINE HAPA

Liverpool manager Jurgen Klopp


Arsenal na Liverpool zinakutana leo katika mchezo wa ligi kuu,
timu zote zikiwa zinasummbuliwa na majeruhi wengi Arsenal itaendelea kumkosa Alexis naCarzola  na wengine na Liverpool inaweza kuwacheza wachezaji wake waliokuwa majeruhi Ibe,Jordan Henderson na Millner

Tokeo la picha la PREMIER LEAGUE LOGO

Mechi Nyingine 

Friday, January 8, 2016

SERIKALI YATOA PICHA MAALUMU YA RAISI JOHN POMBE MAGUFULI KWA MATUMIZI YA OFISI BINAFSI NA SERIKALI

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maelezo na Habari Zamaradi Kawawa akiongea na waandishi wa Habari leo alionyesha picha rasmi ya Mh John Pombe Magufuli ambayo ndio itakayotumika katika ofisi zote za binafsi na serikali.Kwa maelezo ya Kaimu Mkurugenzi huyo picha hiyo itauzwa kwa gharama ya shs 15,000 tu bila Fremu.Pia alitoa onyo kwa wale wanjanja wa kucopy na kupaste kuwa picha hiyo itapatikana katika taasisi hiyo ambayo ndio inamaamlaka ya kuuza picha hiyo.

Dar es salaam.

Habari Maelezo Mtaa wa Samora.

Mikoani

Kwa wakala wa manunuzi serikali kwa mikoa yote. 


Zamaradi Kawawa.


Thursday, January 7, 2016

KAMA HUJUI SAMATTA NDIYE MCHEZAJI BORA AFRICA ABEBA TUZO JANA USIKU

Mchezaji wa kimataifa kutoka Tanzania Mbwana Ally Samatta amefanikiwa kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka ndani ya Afrika.Hakika Samatta ameweza kuwa shujaa na mwanamapinduzi wa ukweli nje ya Tanzania haya ni mafanikio binafsi lakini kwa Taifa pia limepata faida kubwa.

Ni wakati sasa kwa wachezaji wengine kujiwekea malengo kuweza kuvuka record hii ya Samatta ambaye kwa habari za sasa anaacha na TP Mazembe ili kwenda Ulaya kama dili zake zitafanikiwa.Na hivyo anaweza kuja kukaa tena meza moja kugombea zawadi ya kuwa mchezaji bora nje ya Afrika kama tulivyo ona kina Toure,Etoo n.k.Na hakika kwa matazamo wa Samatta atafanikiwa.

12407463_1651933801734351_1469028646_n

SIMBA YAWAFUNGA WAKUSANYA MAPATO WA UGANDA(URA)

Simba jana usiku iliweka matumaini ya kusonga mbele zaidi katika mashindano ya Mapinduzi yanayofanyika Zanzibar baada ya kuifunga URA bao 1 bila na kukusanya pointi 4 mpaka sasa.

Ibrahim Ajib ndie aliyekuwa shujaa wa jana baada kufunga goli safi katika kipindi cha kwanza.Ajib alipiga shuti la mbali ambalo lilimshinda kipa wa URA.Kipa wa Simba nusura awazawadie URA goli baada ya kushika mpira aliorudidhiwa na kuwapa URA nafasi ambayo walishindwa kuitumia.Mpaka kipindi kinaisha Simba 1 URA 0.

Tokeo la picha la ajib ibrahim

Monday, January 4, 2016

CHELSEA YAANZA JEURI TENA,MADRID YASHIKWA NA VALENCIA

Chelsea jana walishinda goli tatu dhidi ya Crystal Palace wakicheza soka safi Oscar dk 29,Willian dk 60 na Costa dk 66 walistosha kabisa kuisambaratisha timu jeuri hiyo.

Willian scores for Chelsea

Huko Hispania Real Madrid na Valencia walishindana nguvu na kutoka sare ya 2-2.Huku Bale na Ronaldo wakikosa nafasi muhimu baada ya kushindwa kuwasiliana na kufanya Madrid ikiendelea kusotea nafasi ya tatu.Huku magoli ya wenyeji yakifungwa na Parejo na Alcacer na wageni Bale na Benzema 

Gary Neville

Wednesday, December 30, 2015

MKALI WA WIMBO WA DURO TOKA NIGERIA TENKOMILES YUPO DAR KWA MKESHA WA MWAKA



Mkali wa Tenkomiles toka Nigeria yupo jijini Dar tayari kuwasha moto katika tamasha la mkesha wa mwaka litakalofanyika ndani ya ukumbi wa Kingsolomoni.Jamaaa akiwa anatamba na wimbo wake wa DURO.

Hakika si pakukosa ili uwezw kufunga mwaka 2015 vizuri kwa burudani kutoka kwa mkali huyo huku tiketi ni 40,000/= kabla ya saa tisa na baada ya hapo ni 70000/=.

LIVERPOOL YAIPIGA SUNDERLAND

Liverpool players celebrate

Christian Benteke shujaa akiwa na kundi la wachezaji wenzake baada ya kufunga goli.

Liverpool jana usiku waliishinda Sunderland kwa goli moja na kufikisha point 30 sawa na Manchester United.Shujaa wa jana alikuwa raia wa Ubelgiji Christian Benteke katika dk ya 46 alipofunga goli safi na kuipa Liverpool ushindi muhimu.

Christian Benteke

Benteke akishinda goli.


MANCHESTER CITY YATOSHANA NGUVU NA LEICESTER

Man city jana usiku ilishindwa kupata pointi tatu kutoka kwa Leicester baada ya kutoka sululu.Matokeo hayo yamekuwa faraja kubwa kwa Arsenal ambayo inaendelea kushika usukani wa Ligi hiyo.

Leicester v Manchester CityMtifuano kati ya wachezaji wa man city na leicester

Sunday, December 27, 2015

MBWANA SAMATTA KARIBU KUTUA UBELGIJI KATIKA KLABU YA GENK

Hatimaye Mbwana Samatta anaweza kucheza ligi ya Ubelgiji katika klabu ya Genk na kuweza kutimiza ndoto yake ya kucheza ulaya kwa mara ya kwanza.Mbwana Samatta safari yake haikuwa rahisi kama tunavyoweza ila bidii ndio imemfikisha hapo alipo kukaa ndani ya Timu yenye vipi tofauti TP MAZEMBE si mchezo hatuna budi kumtakia heri kama atafanikiwa kwenda GENK.

Tokeo la picha la mbwana samata