Showing posts with label education. Show all posts
Showing posts with label education. Show all posts

Tuesday, March 1, 2016

WALIMU KUFUTIWA NAULI DAR NI MOJA YA HATUA YA KUBORESHA AU CHANGAMOTO MPYA

Kuanazia leo lile tamko la Mkuu wa wilaya Bwana Makonda kuwa walimu katika wilaya Kinondoni wataweza kupanda mabasi bure kuanzia saa kumi na moja mpaka saa mbili na saa tisa mpaka kumi na moja jioni.Wengi wametoa maoni yao kuwa ni hatua nzuri katika kuboresha na kujali taaluma hii ambayo bado haina kipao mbele kikubwa katika nchi yetu licha ya kuwa ni nguzo muhimu katika maendeleo ya nchi yoyote duniani.Kwa miaka mingi kumekuwa na vilio juu ya maslahi yao ila mambo bado ni magumu sana.Tumaini langu kuwa kama huyu ameweza kuona hili itafika siku yataonwa na mengine lengo nikuweza kubadilisha hali ya walimu wetu.
Licha mtazamo huo wengine wamebeza na kusema hicho ni kitu kidogo sana kwani walimu wanayo matatizo zaidi ya hayo ni kweli na yanajulikana.Je tukiacha hayo nionavyo mimi inaweza ikawa changamoto mpya hasa kama kwa Makonda wa mabasi hao kuwa chanjo cha kuwatenga na kuwasema vibaya wale ambao tumezoea usafiri huu tunajua Makonda walivyo na maneno ya kashfa na jambo hili jema likwa shuburi licha la kupitishwa na wamiliki wao.Wito yapashwa elimu juu ya hili itolewe vizuri ili lisije likaeleweka vibay na kuwazalilisha walimu wetu wanaofanya kazi nzito na isihishie kuwa amri tu.Natumaini ipo siku walimu wataona faraja na kuthaminiwa zaidi.
Tokeo la picha la teachers in Tanzania photo

Friday, January 22, 2016

KIINGEREZA BADO CHANGAMOTO KATIKA UFAULU

Lugha ya  kiingereza bado imekuwa mtihani mkubwa katika elimu ya Tanzania na hii inaweza kuonekana katika ngazi zote za elimu nchini Tanzania bado uelewa na ufaulu wake umekuwa mdogo sana.

Matokeo ya darasa la nne yametoka na soma ambalo wanafunzi wamefanya vibaya ni somo la Kiingereza ambapo ufaulu wake ni asimilia ndogo chini ya 60 ukilinganisha na masomo mengine yenye ufaulu wa zaidi ya asilimilia 80.

Tokeo la picha la primary students in tanzania 

Wednesday, January 20, 2016

Waziri wa Elimu afutilia mbali mfumo wa GPA.

Tokeo la picha la ndalichako

Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Mafuzno ya Ufundi ameamua kurejesha mfumo wa zamani wa Madaraja(Divion) badala wa uliokuwa unatumika sasa wa GPA.Hii imekuja baada ya kuwapa NECTA muda wa kupitia mfumo huo sasa na waje na sababu za kisayansi kwani mfumo huo unatumika

Waziri akitoa tamko alieleza baadhi ya mapungufu ya mfumo wa GPA 

1.Mgongano wa mkubwa katika kupanga GPA kuanzia sekondari mpaka vyuo vya ualimu

2.Ufinyu wa uelewa kwa watahiniwa kwani viwango vya kufaulu vimeshuka

3.Wadau hawakuhusishwa katika kuratibu mfumo huyo utumike,hata kamishina wa elimu hajatoa kibali.

Hivyo Prof J Ndalichako ameamua kurudisha mfumo wa zamani wa madaraja.Lakini serikali kupitia wizara hii inahitaji kurekebisha mambo mengi ya msingi katika elimu ambayo imekosa mvuto na kuanza kukosa mvuto.Mambo ni mengi sana ambayo yanapelekea kudorora kwa elimu kubwa ni sera mbovu za mawaziri wanaokalia kiti hiki wengi wanaongoza kisiasa na sio kiataaluma wakati research zinaweza fanyika lakini hamna wa kufuatilia.Hata hivyo mazingira ya elimu kwa upande wa walimu na wanafunzi na vitendea kazi bado nis shida ndio maana kuna hitajika nguvu ya ziada.Kama Waziri ameonyesha nia ya sayansi itumike katika kufanya maamuzi juu ya elimu kunaweza kuwa na tija tuwape muda watimize malengo yao.

Thursday, December 3, 2015

SERIKALI YASITISHA KUPANDA KWA ADA SHULE ZA BINAFSI

Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imetoa tamko kuhusiana na ongezeko la ada linalofanywa na shule binafsi kila mwaka.Hivyo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ameomba wamiliki wasitishe ongezeko hilo mpaka serikali itakapo toa ada elekezi kwa shule hizo

Wananchi ambao wana watoto katika shule hizi wamekuwa wanalalamikia ongezeko na ada kubwa zinazotozwa na shule hizo kwa kipindi kirefu.Neema inawezwa kutangazwa na kuweza kuwapa wazazi wengi fursa ya kuwasomesha watoto wao katika shule bora.

Tokeo la picha la tusiime school

Wednesday, December 2, 2015

VINARA WA RUSHWA(UFISADI) BARANI AFRIKA KWA SASA.

Hali ya ufisadi barani Africa imekuwa sugu kwa mataifa mengi viongozi wa serikalini wamekuwa  wakituhumiwa katika kashfa mbali mbali za ufisadi.Nchi nyingi zimeonyesha nia ya kupambana na ufisadi ikiwemo Kenya,Nigeria na Tanzania huku hatua mahususi zikichukuliwa kukabiliana na ufisadi kama kuwafukuza kazi na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wale wote waliobainika na ufisadi.

Shirika la TRANSPARENCY INTERNATIONAL kwa mara kwanza imebainisha kuwa wafanyabiashara ndio MAFISADI wakubwa barani Afrika na maafisa wa polisi kuwa ni vinara.Wananchi wamekuwa wakihitajika kutoa hongo ili waweze kupata huduma muhimu jambo ambalo limekuwa chanzo cha umaskini mkubwa sana katika bara hili.

Nchi inayoongoza Afrika kwa sasa ni Liberia huku Cameroon,Nigeria na Siera Leone zikifuata.Nchi za Botswana,Mauritius na Cape Verde zikiwa na asilimia chache kabisa za ufisadi.Hili ni nyanga Afrika mikakati inahitajika kutokemeza hili.

Tokeo la picha la photos to show corruption
Kataa Rushwa kwa nguvu zote.

Thursday, November 26, 2015

WASOMI WAMWOMBA RAISI MAGUFULI KATIKA UONGOZI WAKE AJALI TAFITI ILI NCHI IPATE MAENDELEO YA KWELI

Wasomi wa Tanzania kwa muda mrefu wameshindwa kuhusishwa kikamili katika kusaidia nchi kupiga hatua kubwa ya maendeleo.Hii inatokana na serikali kwa kipindi kirefu kutochukua hatua ya kujali tafiti mbali mbali ambazo wana taaluma nchini wamekuwa wakizifanya lakini hazifanyiwi kazi na kubaki katika mafaili tu.

Hivyo wanataaluma wamesifia kasi ya magufuli ila wameimuomba kama atakuwa anajali na kufanyia kazi tafiti katika maeneo tofauti zinazofanya na wanataaluma wa kitanzania basi nchi inaweza kupiga hatua kubwa kimaendeleo.Kwani tafiti hizi zitatoa majibu ya matatizo yanayoikabili nchi yetu na zikifuatiliwa kikamilifu maendeleo ya uhakika yatapatikana.Kwani kwa nchi nyingi ambazo zimeweza kuendelea basi tafiti ilikuwa ni chachu ya kufikia maendeleo hayo.Raisi Magufuli chukua ushauri huyo na ufanyie kazi.

Tokeo la picha la images of research and development in africa

Thursday, November 12, 2015

CONVOCATION WIKI YA CHUO CHA BIASHARA(CBE) YAENDELEA

Kuelekea kwenye mahafali siku ya jumamosi Chuo Cha Biashara(CBE) kimekuwa katika wiki ya makongamano mbali mbali ili kuelezea ummma nini kinafanya.Mara nyingi huu umekuwa ni utaratibu wa vyuo vingi kuufanya kabla ya kuhitimishwa na siku ya maahafali ambapo wahitimu katika idara tofauti tofauti wanatunikiwa vyeti kuhitimisha kumalizika kwa ngazi fulani ya kitaaluma mfano Shahada au Stashada n.k.Hivyo ndani ya wiki hiyo kunakuwa na uwakilishwaji wa maandiko mbali mbali,kukutana na wanafunzi walio maaliza (alumni),maonyesho na pia ni wiki ambayo wale wanafunzi waliofanya vizuri wanatunikiwa zawadi.

Chuo cha biashara kitafanya mahafali yake siku ya Jumamosi 14-11-2015 pale Diamond Jubilee Hall.

Tokeo la picha la images of chuo cha biashara logo


Saturday, October 24, 2015

HATIMAYE KARO KUTOPANDA TENA 2016 KWENYE VYUO VIKUU AFRIKA KUSINI


Tokeo la picha la zuma images

Jacob Zuma-Rais wa Afrika Kusini

Rais Zuma wa Afrika Kusini ameutangazia umma wa wanafunzi walio kuwa nje ya ofisi yake  kuwa karo kwenye vyuo vikuu haitaongeka tena baada ya maandamo makubwa kutokea nchini humo tangu kumalizika kwa ubaguzi wa rangi 1994.Kabla ya hapo ilipendekezwa serikali ilikubali kuongeza ada kwa 6% kupinga ile ya iliyopendekezwa na wasimamizi wa vyuo kati ya 10% na 12%.Hivyo basi hakutakuwa na ongezeko lolote kwa mwaka wa masomo 2016.Kweli mabadiliko yanahitaji umoja wameweza bila ya kuangalia tofauti zao kati ya Raia wenye  asili ya kizungu na kiafrika wote walijumuika katika maandamo hayo.

Tokeo la picha la students riot in south africa images


Tokeo la picha la students riot in south africa images

Tokeo la picha la students riot in south africa images

Wanafunzi wakiwa katika maaandamo kabla ya kukubaliwa ombi lao.


Thursday, October 1, 2015

MIKAKATI KWA WAHITIMU WA VYUO VIKUU JUU YA MAISHA BAADA YA CHUO

Twaweza sema tatizo la ajira sasa linakuwa janga ndani ya serikali nyingi za africa huku wahitimu wengi wakiwa wanahaha kutafuta ajira ambazo zimekuwa ni adimu sana katika kipindi hiki.Hii imepelekea serikali nyingi kuelekeza wahitimu watumie fursa walizo nazo waweze kujiari.Hivyo kuelekea hili vyuo 16 vya Afica vimekutana mjini Arusha kupanga mikakati jinsi ya kuwasaidia vijana wanaohitimu katika vyuo,waweze kujiajiri badala ya kusubiri ajira pekee.Hakika hili linapaswa kusimamiwa ili kubadili akili za wahitimu wengi ili kuwafanya wajisiri na kuweza kujiari na kupunguza tatizo la ajira

HABARI NJEMA NACTE YAONGEZA MUDA YA KUDAHILI WANACHUO

NACTE imesogeza muda wa kudahili wanafunzi wanao jiandaa kujiunga na vyuo vikuu ili kuwapa muda zaidi wanafunzi ili waweze kushiriki katika uchaguzi wa 25-10-2015.Hivyo imetoa wito kwa vyuo vyote ambavyo vipo chini yake vifungwe kwa wiki mbili kuwapa wanafunzi muda wa kujiandaa kupiga kura.Sasa wanafunzi wataendelea kujisajili kupitia mfumo wa CAS mpaka 16-10-2015 na vyuo kufunguliwa Novemba haya yameelezwa leo na Kaimu Katibu Mtendaji NACTE Bw. Adolf Rutaiyuga