Showing posts with label political. Show all posts
Showing posts with label political. Show all posts

Monday, February 8, 2016

Hili la Zanzibar linahitaji hekima ya juu lifikie mwafaka

Hali ikiwa bado si shwari sana visiwani Zanzibar huku tarehe ya uchaguzi ikiwa imeshatolewa na Tume ya Uchaguzi.CUF wakitoa tamko la kutoshiriki uchaguzi huo bado ni tamko tete hasa hasa.Huku baadhi wanasheria wakitoa mitazamo hayo juu ya hii.

Jambo la msingi ni kupata hekima na busara  baina ya pande zote zinazosuguana kwani haki isipotendeka lolote baya laweza tokea.Haya yote kwa maono yangu yatafikia tamati kama sheria    itaingilia kati katika kupata haki kati ya hizi pande mbili ili mgogoro huu unaoendelea uweze kupita salama.

Tokeo la picha la zanzibar view

Friday, January 22, 2016

TAREHE YA KURUDIA UCHAGUZI ZANZIBAR YAWEKWA WAZI

Habari za hivi punde tume ya uchaguzi chini ya Jecha imetangaza siku ramsi ya marudio ya uchaguzi mkuu Zanzibar kuwa ni Machi 20,2016.

Uchaguzi utahusisha:
1.Uchaguzi wa Raisi

2.Wajumbe wa baraza la wawakilishi

3.Madiwani

Hivyo katika kipindi hakutakuwa na uteule mpya wa wagombea wala kampeni.

Tokeo la picha la JECHA

Wednesday, January 13, 2016

DR SHEIN ATOA MATUMAINI MAPYA SIKU YA MAPINDUZI YA MIAKA 52 JANA,SEIFU AKACHA

Tokeo la picha la dr shein

Hali ya siasa ya Zanzibar bado haiko sawa hasa baada ya Maalim Seifu Makamu wa Raisi kusema hatoweza kuhudhuria sherehe hizo.Dr Shein ambaye katiba bado inamtambua kama Raisi halali wa Zanzibar jana alitoa matumaini mapya baada ya kuwaeleza umma wa wananchi wa Zanzibar kuhusu mzozo wa kisiasa kuwa mpaka sasa hivi mazungumzo yako katika hatua nzuri na uchaguzi utafanyika tena kulingana na katiba inavyosema hivyo wananchi wanapaswa kusubili tarehe rasmi ya kupiga kura.

Wednesday, December 30, 2015

RAISI MAGUFULI ATEUA MAKATIBU NA MANAIBU ZAIDI YA 50,HUKU MAPFOFESA NA MADOKTA WAKIONGOZA


Tokeo la picha la RAISI MAGUFULI

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa makatibu wakuu na manaibu Katibu wakuu katika Wizara mbalimbali.
Walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
1. Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi - Ombeni Sefue

2. Katibu Mkuu Ikulu
Peter Ilomo

3. Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora
Dkt. Laurian Ndumbaro

4. Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Mhandisi Mussa Iyombe (Katibu Mkuu)
Dkt. Deo Mtasiwa (Naibu Katibu Mkuu - Afya)
Bernard Makali (Naibu Katibu Mkuu - Elimu)

5. Ofisi ya Makamu wa Rais
Mbaraka A. Wakili ( Katibu Mkuu)
Mhandisi Ngosi Mwihava (Naibu Katibu Mkuu)

6. Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge, Sera, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu)
Erick Shitindi (Katibu Mkuu Kazi na Ajira)
Mussa Uledi (Katibu Mkuu Bunge)
Dkt. Hamis Mwinyimvua (Katibu Mkuu - Sera)

7. Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Dkt. Frolence Turuka (Katibu Mkuu - Kilimo)
Dkt. Mashingo (Katibu Mkuu Mifugo)
Dkt. Budeba (Katibu Mkuu - Uvuvi)

8. Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Mhandisi Joseph. Nyamuhanga (Katibu Mkuu - Ujenzi)
Dkt. Leonard M. Chamuliho (Katibu Mkuu - Uchukuzi)
Profesa Faustine R. Kamuzora (Katibu Mkuu - Mawasiliano)
Mary Sassabo (Naibu Katibu Mkuu Mawasiliano)

9. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Dkt. Yamungu Kayandabira (Katibu Mkuu)
Dkt. Moses Kusiluka (Naibu Katibu Mkuu)

10. Wizara ya Maliasili na Utalii
Meja Jenerali Gaudence S. Milanzi (Katibu Mkuu)
Anjelina Madete (Naibu Katibu Mkuu)

11. Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
Dkt. Adelhem James Meru (Katibu Mkuu - Viwanda)
Profesa Adolf F. Mkenda (Katibu Mkuu - Biashara na Uwekezaji)
Mhandisi Joel Malongo (Naibu Katibu Mkuu)

12. Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.
Maimuna Tarishi (Katibu Mkuu)
Profesa Simon S. Msanjila (Naibu Katibu Mkuu)
Dkt. Leonard Akwilapo (Naibu Katibu Mkuu)

13. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Dkt. Mpoki Ulisubisya (Katibu Mkuu - Afya)
Sihaba Nkinga (Katibu Mkuu - Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto)

14. Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
Profesa Elisante Ole Gabriel Mollel (Katibu Mkuu)
Nuru Halfan Mrisho (Naibu Katibu Mkuu)

15. Wizara ya Maji na Umwagiliaji
Mhandisi Mbogo Futakamba (Katibu Mkuu)
Mhandisi Kalobero Emmanuel (Naibu Katibu Mkuu)

16. Wizara ya Nishati na Madini
Profesa Justus W. Ntalikwa (Katibu Mkuu)
Profesa James Epifani Mdoe (Naibu Katibu Mkuu)
Dkt. Paulina Pallangyo (Naibu Katibu Mkuu)

17. Wizara ya Katiba na Sheria
Profesa Sifuni Mchome (Katibu Mkuu)
Suzan Paul Mlawi (Naibu Katibu Mkuu)
Amon Mpanju (Naibu Katibu Mkuu)

18. Wizara ya Mambo ya Ndani
Jaji Meja Jenerali Projest A. Rwegasira (Katibu Mkuu)
Balozi Hassan Simba Yahaya (Naibu Katibu Mkuu)

19. Wizara ya Fedha na Mipango
Dkt. Silvacius Likwelile (Katibu Mkuu)
Dorothy Mwanyika (Naibu Katibu Mkuu)
James Dotto (Naibu Katibu Mkuu)
Amina Hamis Shaban (Naibu Katibu Mkuu)

20. Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa
Dkt. Aziz Mlima (Katibu Mkuu)
Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi ( Naibu Katibu Mkuu)

21. Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Job D. Masima (Katibu Mkuu)
Immaculate Peter Ngwale (Naibu Katibu Mkuu

Makatibu wakuu na Manaibu Katibu Wakuu wote ambao hawajatajwa katika orodha hii watapangiwa kazi nyingine.

Katika hatua nyingine Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Eliakimu Maswi kuwa Kaimu Naibu Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na ametengua uteuzi wa Naibu Kamishina wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Bw. Lusekelo Mwaseba, ambaye atapangiwa kazi nyingine

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
30 Desemba, 2015

Monday, December 28, 2015

MAGUFULI AWAAPISHA KINA MAGHEMBE NA WENZAKE KUANZA KAZI RASMI

Raisi Magufuli leo amewaapisha Mawaziri na Manaibu ambao aliwateua katika zile Wizara ambazo zilikuwa bado hazijapata watendaji hao.Mawaziri hayo ni

1.Profesa J Maghembe-Waziri Maliyasili na Utalii

2.Dkt Philip Mpango-Waziri wa Fedha na Mipango

3.Mhandishi Gerson Lwenge-Waziri Maji na Umwagiliaji

4.Dkt Joyce Ndalichako-Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi

5.Hamad Masauni-Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi

6.Prof Makame Mbarawa-Waziri ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano.

Maghembe akila kiapo

Mawaziri wapya kabla kuapishwa.



Saturday, December 12, 2015

NCHI YAANZA KWENDA MCHAKAMKA BAADA YA MAWAZIRI KUAPISHWA JANA,SIKIA BAADHI YAO NA KAULI ZAO


Siku ya Jumamosi ilikuwa ni siku maalumu kwa Mawaziri na Manaibu Mawaziri kula kiapo kama ishara ya kuanza kazi ramsi chini ya kauli MBIU HAPA KAZI TU.Baada tu kuapishwa mawaziri walitoa matamko.


1.William Lukuvi-Waliojenga maeneo yasiyo rasmi waanze kutekeleza wajibu wao

2.Dr Kigwangala-Board yote ya hospitali ya Amana tukutane kesho saa 10 Wizarani kwa maelekezo zaidi

3.Ummy Mwalimu-Vyandarua vinunulie katika hospitali ya Mwananyamala na maboresho yafanyike haraka

4.Muhongo-Kasi ya umeme vijijini itarudi pale pale,bei itashuka ya umeme na kazi ifanyike kwa vitendo

5.Kairuki-Tehema itumuke katika mahudhurio ya wafanyakazi waachane na madaftari

6.Nape haki za wasanii zitalindwa

 


Thursday, December 10, 2015

RAISI MAGUFULI ATANGAZA BARAZA LA MAWAZIRI NA KUWAAMBIA WANA KAZI NGUMU


BARAZA LA MAWAZIRI
Wizara ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora
Mawaziri – George Simbachakene  na Angella Kairuki
Naibu Waziri – Sumeilam Jafo. Naibu
Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Raisi, Muungano na Mazingira
Waziri – January Makamba
Naibu Waziri – Luhaga Jerrson Mpina
Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu
Waziri – Jenista Muhagama
MaNaibu – Dkt. Possy Abdallah na Anthony Mavunde
Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Waziri – Mwigulu Nchemba
Naibu Waziri – William Ole Nasha
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Waziri Bado hajapatikana.
Naibu Waziri – Inj. Edwin Ambandusi Ngonyani
Wizara ya Fedha na Mipango
Waziri Bado hajapatikana.
Naibu Waziri – Ashantu Kizachi
Wizara ya Nishati na Madini
Waziri – Prof. Mwigalumi Muhongo
Naibu Waziri – Medalled Karemaligo
Wizara ya Katiba na Sheria,
Waziri – Harrison Mwakyembe
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa
Waziri – Dk. Augustino Mahiga
Naibu Waziri – Dkt. Susan Kolimba.
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Waziri – Dk. Hussein Mwinyi
Wizara ya Mambo ya Ndani
Waziri – Charles Kitwanga.
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Waziri – William Lukuvi
Naibu Waziri – Angelina Mabula
Wizara ya Maliasili na Utalii
Waziri Bado hajapatikana
Naibu Waziri– Inj. Ramol Makani
Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Waziri Charles Mwijage.
Wizara ya Elimu,Sayansi Teknolojia na Ufundi
Waziri Bado hajapatikana.
Naibu Waziri – Inj. Stella Manyanya
Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Waziri – Ummy Mwalim
Naibu Waziri –  Dkt. Hamis Kigwangala
Wizara ya Habari, Utamadu, Wasanii na Michezo
Waziri – Nape Nnauye
Naibu Waziri – Anastasia Wambura
Wizara ya Maji na Umwagiliaji
Waziri – Prof. Makame Mbarawa
Naibu  Waziri– Inj. Isack Kamwela

Wednesday, December 2, 2015

RAISI PAUL KAGAME KATIKA PRESHA NA LISTI YA MARAISI WALIOKAA MUDA MREFU

Raisi Paul Kagame wa Rwanda amepitishwa tena kuwania kitu cha uraisi na senata  baadaye 2017 baada ya awamu ya pili kuisha,hivyo atakuwa na uwezo wa kuongoza tena Rwanda kwa awamu ya tatu.Uwamuzi huyo umepigwa vibaya na Marekani kupitia Balozi wake akimwomba Raisi Kagame awe kiongozi bora kwa kuheshimu katiba na kuachia madaraka ifikapo 2017 muda wake utakapoisha.

Tatizo hili limekuwa na mizizi hasa katika bara la Afrika Maraisi wengi wamekuwa wakibadili katiba ili kuweza kupata muda zaidi za kuendelea kuwa Maraisi.Tumeshuhudia nchi nyingi zikiingia kwenye vita  na baadhi ya serikali kupinduliwa kama Sierra Leone.Burundi mapigano yanaendelea huku Raisi Nkurunzinza akijiongezea muda wa kuongoza bila ya kujali maisha ya raia wanakufa na kukimbia nchi yao kila siku.Baadhi ya maraisi waliokaa madarakani muda mrefu ni (1). Teodora Obiang Nguema Mbasogo -Equatorial Guinea Madarakani Miaka 32 (2). Jose Eduardo Dos Santos –  Angola Madarakani miaka 32 (3). Robert Mugabe – Zimbabwe Madarakani Miaka 31 (4). Paul Biya – Cameroon Madarakani  Miaka 29 (5). Yoweri Museveni – Uganda Madarakani Miaka 25 (6). King Mswati III – Swaziland Madarakani Miaka 24 (7). Blaise Compore 24 (8) Kagame 19

Katika kukomesha hili Balozi wa marekani amemwambia Raisi Kagame aaichie madaraka muda ukifika.Na hili lilisitizwa na Barack Obama kuwa hamna haja ya kupenda kuwa Raisi kwani changamoto haziwezi kuondolewa na mtu mmoja alipokuwa akihutubia Umoja wa nchi za Kiafrica -Addis Ababa.Sioni tatizo Maraisi kufanya hivyo hasa Afrika mbona nchi zilizoendelea ni jambo la kawaida na maisha yanaendelea kuimarika kwa wanancghi wao, kinyume na Viongozi wa Afrika cha msingi ni kuweka misingi ya kitaifa iliyoimara na kuweza kuamini mtu fulani ndio kiongozi sahihi kwa mu muda mrefu.


Tokeo la picha la kagame
Raisi Paul Kagame na Mkewe

Raisi wa Burundi Pierre Nkurunziza ambaye amerejea nchini mwake baada ya kushindikana kwa jaribio la mapinduzi ya kijeshi
Raisi Pierre Nkurunzinza.-Burundi.

Thursday, November 26, 2015

SERIKALI YA AWAMU YA TANO NI NOMA

Serikali ya awamu ya tano imetoa maelekezo mengine kama hatua ya kubana matumizi baada ya kutoa tamko kuwa mwaka 2015 serikali haitaingia gharama za uchapishaji kadi za XMAS AND NEW YEAR kama ilivyozoeleka.Hivyo matumizi hayo yataelekezwa kwenye mambo muhimu ya kijamaa.Taarifa hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa mawasiliano Gerson Msigwa.

Thursday, November 19, 2015

HATIMAYE KASSIM MAJALIWA NDIYE WAZIRI MKUU WA TANZANIA


Tokeo la picha la images of majaliwa
Raisi wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania mweshimiwa Dkt John Joseph Pombe Magufuli amemteua Ndugu Majaliwa Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu mteule.Kwa ufupi Waziri mteule aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Tamisemi na pia ni Mbunge wa Jimbo la Ruangwa,kitaaluma ni mwalimu na pia aliwahi kushika nyadhifa mbali mbali serikalini kama mkuu wa wilaya.Mh Majaliwa amepitishwa kwa asilimia 73% kwa kura zilizopigwa na Wabunge .
Kesho kulingana na taarifa za Mh Spika Job Ndugai waziri huyo mteule ataapishwa katika Ikulu ndogo ya Chamwino na Raisi.


Tuesday, November 10, 2015

MEMBE ALETA MPYA BAADA YA RAISI MAGUFULI KUFUTA SAFARI ZA NJE

Tokeo la picha la bernard membe images


Baada ya hatua ya Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kusitisha safari za nje na kuamua balozi katika nchi husika wataratibu shughuli zote kwa niaba ya nchi.Aliye kuwa Mbunge na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe amepiga amesea ilikuwa inatisha KWANI WATU WALIKUWA WANAENDA NJE KAMA KARIAKOO hivyo ameunga mkono hatua hiyo na kusema itapunguza matumizi ya serikali kwa kiasi kikubwa.Ni hatua ambayo kila mwananchi wa Tanzania ameungana nayo kwani safari nyingi zilikuwa hazina tija kwa Taifa bali kuongeza gharama na mzingo kwa taifa letu.

Monday, November 9, 2015

HATMA YA VIONGOZI WA SERIKALI ZANZIBAR BADO TATA

Huku Katiba ikimpa mamlaka Dkt Shei kuendelea kuongoza serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.Utata umekuja juu ya mawaziri wake katika hali hiyo baadhi ya Mawaziri waliokuwa wameshikilia wizara mbalimbali Visiwani hasa wale wa CUF wamesema kisheria  wao sio viongoza si tena.Ni zaidi sasa wa wiki mbili mbili swala la Zanzibar  linapata sura mpya kula kukicha huku Chama Cha Wananchi (CUF) kikataa hatua ya Mwenyekiti wa Tume ndugu Jecha kufuta uchaguzi na baadala yake wanaomba tume hiyo itumie busara kuwapa ushundi wao kwani hata baadhi ya Wawakilishi walishapewa vyeti vyao vya ushindi na tume hivyo sio hali kupinga ushindi walioupata.

Tokeo la picha la images of zanzibar citiznes

RAISI BUHARI KAMA RAISI MAGUFULI WA TANZANIA AMPIGA CHINI MKURUGENZI WA KUPAMBANA NA RUSHWA

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amemfuta kazi mkuu wa Taasisi ya kupambana na Rushwa nchini humoa ndugu Ibrahamu Lamorde ambaye ameshikilia wadhifa huo tangu 2011.Hadi sasa Raisi huyo bado hajawaapisha mawaziri wake inatarajia wiki hii zoezi hilo linaweza kufanyika.

Tokeo la picha la buhari president

RAISI MAGUFULI KWA HILI NAKUPA TANO

Tokeo la picha la images of magufuli

Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania


Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mweshimiwa John Pombe Magufuli hivi karibuni katika kikao chake na Makatibu na Maanaibu Makatibu wakuu na baadhi ya viongozi katika Taasisi kubwa kama Mamlaka ya Mapato na Benki kuu ya Taznania.Mambo mengi yalizungumza hasa lililo nigusa ni hatua yake ya kukata safari zote za nje kwa viongozi mbalimbali wa serikalini.Hii ni hatua nzuri katika kupunguza matumizi makubwa ya serikali.Ni vyema sasa viongozi wetu wajenge tabia ya kufanya kazi  na sio kutafuta mianya ya kujiongezea vipato kwa njia halali kama hizi lakini zisizo na tija kwa Taifa kwani viongozi wengi serikalini kwa muda mrefu wamekuwa wakitumia fursa hii zaidi katika manufaa yao binafsi kuliko kwa Taifa kwani tunaishi nao na tunajua hivyo hongera sana Raisi ongeza kasi zaidi katika mambo mengine kama mashangingi,vikao vya ndani visivyo na tija,rasimali za ofisi kama ambazo zimekuwa hazifuati utaratibu mzuri na kuuongezea serikali gharama zisizo za lazima.

Tunaaamini Hapa kazi Tu kwa manufaa ta Taifa letu.

Thursday, November 5, 2015

MAGUFULI RAMSI RAISI WA TANO WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


Jana ilikuwa siku kubwa nchini Tanzania pale Mh John Magufuli alipoapishwa kuwa Raisi wa Tano wa Tanzania.Mamia ya wananchi walijitokeza kushuhudia hafla hiyo huku viongozi kutoka nchi mbali mbali za kiafrika na mabalozi walikuwepo pia.

Ni hatua muhimu kwa Taifa dogo la Tanzania lenye changamoto nyingi  katika nyanja mbalimbali.Nasema ni hatua muhimu hasa katika kipindi cha miaka 10 tumeshudia wanatanzania wengi wakikata tamaa ndani ya nchi yao nakuhitaji mabadiliko ya kweli.Mh Raisi alitoa ahadi nyingi huku akisisitiza mabadiliko katika uongozi hakika uchaguzi umeisha salama na John Pombe amekuwa Raisi wa Tanzania.Watanzania wengi wanamatumaini makubwa juu yake hasa kutokana na utendaji kazi wake.

Katika hotuba ya kwanza kabisa kama Raisi ameedelea kusisitza kuwa ahadi alizozitoa atazitimiza kwa uhakika na kumuomba mwenyezi amsaidia katika kutimiza yale watanzania wanayotarajia.Hivyo ni kipindi cha utulivu na kila mmoja wetu afanye kazi kwa bidii ili kuweza kusogeza Taifa letu mbele ndio maana kauli mbiu yake ilikuwa HAPA KAZI TU.



Friday, October 30, 2015

MAGUFULI NA SAMIA WAKABIDHIWA VYETI NA KUAHIDI KUWATUMIKIA WANANCHI KWA DHATI

Raisi Mteule baada ya kupokea cheti kutoka kwa Jaji Lubuva

Raisi Mteule amekabidhiwa cheti chake cha kudhibitisha kuwa mshindi baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika 25-10-2015.Raisi huyo mteule amesema atawatumikia wananchi kwani anadeni kubwa na anaona ugumu wa kazi iliyopo mbele yake.
Ameendelea na kuwapa angalizo watendaji wabovu hatawavumilia hata kidogo hivyo watimize majukumu yao kikamilifu la sivyo atafukuzwa tu.Na yeye atakuwa ni Raisi wa nchi nzima hivyo anaomba wananchi wote wamsaidie.
Akiwa na Mgombea wa ACT Anna.


Baadhi ya sehemu ya wanachama waliokuwepo kwenye ukumbi.

Thursday, October 29, 2015

DUNIA YAISHUKIA ZEC ZANZIBAR,TANZANIA BARA FUKUTO ILA WASUBIRI SAUTI YA MAGUFULI KAMA RAISI MTEULE KWA MARA YA KWANZA



Tokeo la picha la zanzibar zec
Marekani na Uingereza zimeeleza masikitiko yao juu ya utaratibu uliofanywa na ZEC kusitisha
 mchakato mzima wa uchaguzi Zanzibar.Huku wakitoa matamko ya uchaguzi huo uendelee na hamna sababu ya kuwanyima haki Wanzibari.Mpaka sasa hakuna tamko lolote kutoka serikalini kuhusu mchakato na vuguvugu linaloendelea.Tanzania bara Rais mteule wa awamu ya tano Mh John Magufuli bado hajapata muda wa kuzungumza na wananchi hiyo ndio shauku inayo subiliwa kwa hamu kwani jana mitaa mbali mbali ya Tanzania Bara wananchi walijitokeza wakifurahia ushindi huo.Kweli mambo yameisha Bara,tuombe afanye kama alivyoahidi tuwenze kupata mabadiliko ya kweli na sio mbwembwe za kampeni tu.

Mungu  atuongoze na Tunamuombea Magufuli afanye mabadiliko katika Katiba yetu tuweze kuwa na Tume Huru ya uchaguzi na vingine vingi ambavyo vitampa mwananchi uwezo wakusimamia nchi yake tukumbuke DEMOKRASIA ni nguvu ya wananchi ikiwa kinyume kamwe hamna demokrasia.Ni jambo la msingi na hata wasimamzi kutoka Africa Mashariki wametoa angalizo hili.

Tokeo la picha la images of tanzania ccm supporters

UWIZI WA KURA HAITI WASABABISHA MAAANDAMO

Tokeo la picha la haiti voters images

Wanachi wa Haiti wanaosuburi matokeo baada ya kupiga kura kuchagua viongozi wao wa,Waandamanaji hao walijitokeza mabarabarani baada ya mgombea wanaomuunga mkono Moise Jean-Charles, kudai kuwa kura zake zimeteketezwa moto ama kufichwa.Wanaiishtumu tume ya uchaguzi nchini humo kwa kukiuka kanuni na utendaji wa uchaguzi huru na wa haki.Waangalizi wa umoja wa matafa wamesifu utendaji kazi wa tume hiyo ya uchaguzi wakisema kuwa kwa kiasi kikubwa uchaguzi huo ulikuwa wa haki .Hata hivyo maafisa wamepigwa na butwaa baada ya madai hayo ya kuibiwa kura kuibuka na sasa wameanzisha uchunguzi kutathmini ukweli wake.Matokeo ya kimsingi yanatarajiwa kutangazwa juma lijalo.

Tokeo la picha la haiti voters images


Wednesday, October 28, 2015

MAREKANI YATAKA MCHAKATO UCHAGUZI ZENJ UENDELEE,SEIFU ATAKA JUMUIYA KIMATAIFA IINGILIE

Tokeo la picha la embassy of usa in dar es salaam images



Balozi ya Marekani imeomba ZEC iendeleee na mchakato wa kutangaza matokeo ili iwape Wanzanzibari haki yao kwani ni vyema kuheshimu haki yao.Tume ya uchaguzi ilichukua hatua hiyo jana huku ikitoa orodha ya changamato kupelekea kusitisha zoezi zima.Ingawa bado sintofahamu inaendelea kwani Mgombea kupitia CUF Maalim Seif amepinga.Tuombee tu mchakato uendelee na wananchi wapewe haki yao.

HATIMAYE MATOKEO ZANZIBAR YAFUTWA


Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Salim Jecha Salim ametangaza kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi visiwani humo akisema uchaguzi huo ulijaa kasoro nyingi.
Kulingana na mwanahabari wa BBC aliyeko hilo Sammy Awami, mwenyekiti huyo ametangaza hatua hiyo kupitia runinga ya serikali visiwani ZBC.
Bw Jecha amesema kuwa uchaguzi huo haukuwa wa haki na kwamba kulikuwa na ukiukaji mkubwa wa sheria za uchaguzi, kwa mujibu wa taarifa ambayo baadaye imetumwa kwa vyombo vya habari.
Amesema baadhi ya makamishna wa tume hiyo, badala ya kutekeleza majukumu yao inavyotakiwa kikatiba "wamekuwa ni wawakilishi wa vyama vyao".
"Kumegundulika kasoro nyingi katika uchaguzi huu miongoni mwa hizo ni kubainika kwa baadhi ya vituo hasa Pemba vimekuwa na kura nyingi kuliko daftari la wapiga kura wa kituo husika."
Amesema hilo ni jambo la kushangaza ikizingatiwa kwamba "baadhi ya wapiga kura hawakwenda kuchukua vitambulisho vyao vya kupigia kura".
Kadhalika, amesema kura hazikupata ulinzi mzuri hususan kisiwani Pemba ambako amesema kuwa baadhi ya mawakala wa baadhi ya vya vyama vya siasa katika kisiwa hicho walifukuzwa.
Ameongezea kuwa vijana katika eneo hilo walivamia vituo vya kupigia kura kwa lengo la kutaka kuzua ghasia, na pia vyama vya siasa vilionekana "kuingilia majukumu ya tume ikiwemo kujitangazia ushindi na kupelekea mashindikizo kwa tume."
Image captionHii ni sehemu ya taarifa ya Bw Jecha
"Nimeridhika kwamba uchaguzi huu haukiwa wa haki na kuna ukiukwaji mkubwa wa sheria na taratibu za uchaguzi," amesema Bw Jecha.
"Hivyo, kwa uwezo nilionao natangaza rasmi kwamba uchaguzi huu na matokeo yake yote yamefutwa na kwamba kuna haja ya kurudia uchaguzi huu."
Tangazo la mwenyekiti huyo limetolewa huku hali ya wasiwasi ikiendelea kutanda visiwani humo.
Siku moja baada ya uchaguzi kufanywa, mgombea wa chama cha upinzani cha Civic United From (CUF) Seif Sharif Hamad alijitangaza kuwa mshindi, hatua iliyokemewa na chama cha CCM ambacho mgombea wake Dkt Ali Mohamed Shein amekuwa rais wa visiwa hivyo muhula unaomalizika.
Tume ya uchaguzi visiwani humo pia ilishutumu hatua ya mgombea huyo. Kabla ya kufutiliwa mbali kwa matokeo ya uchaguzi, tume hiyo ya uchaguzi ilikuwa imetangaza matokeo ya majimbo 31 kati ya majimbo 54 visiwani humo.
Hayo yakijiri Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania inaendelea kutoa matokeo ya uchaguzi wa urais. Kufikia sasa imetoa matokeo ya majimbo 155 kati ya majimbo 264.