Showing posts with label Economic. Show all posts
Showing posts with label Economic. Show all posts

Monday, May 9, 2016

HUJUMA HIZI SI ZA KUZIACHIA HATA KIDOGO

Wananchi wa Tanzania kwa takribani mwezi mzima wamepata taabu kubwa baada ya sukari kuadimika.Hii imekuja baada matamko ya serikali baada ya kutoa bei elekezi na kusitisha vibali vya uwagizaji bidhaa hii.Baadala ya kutafuta njia mbadala na zilizosahihi wafanya biashara wakaficha sukari wakidhani serikali ingerudi nyuma.Kibao kimewageukia na njama zao potofu hakika rai yangu serikali isimame imara na isirudi nyuma kwa hili,kuteseka huku ni kwa muda wananchi wa hali ya chini ndio waliokuwa na taabika siku zote natumai mipango ya serikali ikikaa vizuri kila mtu atafurahi na wale wanaopinga hatua hizi watakuja kubadilika tuu,mabadiliko yoyote si rahisi kukubalika mapema hivyo tunabudi ya kuyakubali na matunda yataonekana baadaye.

Tokeo la picha la sugar tonnes

Friday, January 22, 2016

BRT KITENDAWILI BADO WAKAZI WA DAR ES SALAAM WAISUBILIA HATMA YAKE KWA HAMU

Licha ya matokeo mengi kuhusu kuanza kufanya kazi kwa mradi wa mabasi yaendeyo kasi Dar es salaam ali maarufu BRT.Hamna wa kutengengua kitendawili ni lini mabasi haya yataanza kazi na kuwapa nafuu wakazi wa jiji la Dar es salaam.Awali ilikuwa katikati ya Desemba ikaja Januari 10.Tarehe zote hizo hakuna kilichotekelezwa huku ikiaminika sasa mradi unaweza chukua muda mrefu sasa.

Tokeo la picha la BRT PHOTO IN TANZANIAWakazi wa dar wakiangalia mradi

Tokeo la picha la BRT PHOTO IN TANZANIA

Labda ingeweza kupunguza adha hii kwa wakazi wa morogoro road kuacha magari yao

Wednesday, January 20, 2016

Hali yaanza kuwa tete ndani ya siku zaidi 70 baada ya Raisi wa awamu ya tano kuapishwa

Tokeo la picha la magufuli
Hapa kazi tuu

Kumekuwa na vilio vya hapa na pale juu ya mwenendo mzima wa kipato cha mtu binafsi ndani ya nchi yetu katika kipindi hichi cha Raisi Magufuli huku wengi wakilalamika maisha ni magumu sana.Mara baada ya Raisi kuingia madarakani kipaombele chake kilikuwa ni kupunguza matumizi yasio ya lazima ndani ya serikali na badala yake fedha ziende kwenye matumizi yenye tija na kukusanya kodi.

Hatua hii ya serikali kutangaza vita hiyo inaonekana kuwa shuburi nzito katika maeneo mbali mbali kwa mfano,Baa ,Hoteli,Catering,Makampuni binafsi.Utafiti unaonyesha kuwa mapato yamepungua kwa kiasi kikubwa hasa na inaoneka hali hii inaweza kuwa tishio kwa ustawi ya sekta hizo.

Nini kinaweza tokea sasa upo uhakika kabisa baadhi ya waajiri kuamua kupunguza wafanyakazi na hivyo kuongeza tatizo la ajira ndani ya nchi.Hata wale ambao walikuwa wamejiari wanaweza kushindwa tena kwani kuna baadhi walitegemea semina na warsha za serikali ili wapate tenda.

Mimi binafsi naamini hali itakuwa sawa tuu hata kipindi cha Mkapa wananchi walipitia hali hii,ni ujinga kuendelea kutumbua hela za serikali na kunufaisha watu wachache kwa dili za semina na warsha zisijo na tija huku hali kwa mwananchi wa kawaida akikosa mahitaji muhimu.Magufuli aeendelee na kasi hii ili wananchi watambue heshima ya kufanya kazi zaidi kuliko kuamini katika njia za mkato zisizo na tija kwa taifa.

Hizo ni siku 70 tuu je ndani ya siku 1750 ya uongozi wake tutakimbia nchi?

Monday, January 18, 2016

BEI YA MAFUTA YAZIDI KUSHUKA HAIJAWAHI KUTOKEA TANGU 2003

Bei ya mafuta imezidi kushuka zaidi katika kipindi hichi cha 2016 hii kwa takwimu inaonyesha ni anguko la kihistoria kutokea tangu 2003 ambapo ilishuka mpaka dola 27.67 kwa pipa.Waatalamu wa uchumi wanabashiri anguko linaweza kuwa kubwa hadi kufikia kati ya dola 28-24 kwa pipa hii inaweza kuwa kwani IRAN nchi inayotoa mafuta kwa wingi kwa sasa imefutiwa vikwazo vyake.Hivyo Iran  inaweza ongeza uzalishaji maradufu kwa mapipa nusu milioni kwa siku,nchi inashika nafasi ya 4 duniani katika utoaji wa mafuta.

Tokeo la picha la photos for oil extraction

Wednesday, January 6, 2016

MAMLAKA YA MAPATO (TRA) YAKUSANYA MAPATO YA KIHOSTORIA,,PROF LIPUMBA ATOA ANGALIZO

Tokeo la picha la TANZANIA REVENUE AUTHORITY BUILDING PHOTO

Kwa mara ya kwanza ndani ya mwenzi mmoja mamlaka ya mapato TRA imewezeka kukusanya mapato ya kodi na kufikia TILIONI MOJA POINTI NNE-(1.4.Hii ni historia kwa TRA kuweza kukusanya fedha zote hizo kwa mwezi ikiwa ni ongezeko la karibuni billioni 400 wanahitaji pongezi ila kasi zaidi ina hitajika.

Wakati huohuo Prof. Ibrahimu Limumba ametoa angalizo kwa TRA kuwa wabunifu zaidi na wasibweteke na makusanyo ya ushuru kupitia bidhaa zinazotoka njee maana upo uwezekano kuwa ongezeko hilo ni baada ya wafanyabiashara kubanwa na kulipa kodi ipasavyo.Hivyo inaweza pia kuwafanya kusitisha kuagiza njee kwani faida waliokuwa wakiipata wanaweza kutoipata tena hivyo ni lazima wigo wa kodi uongezeke na sio kubakia sehemu moja tu.

Friday, December 4, 2015

KAZI IMEANZA 8 WA TRA WAFIKISHWA KORTINI KWA UFISADI

Wafanyakazi wa TRA ambao wamehusika katika upotevu wa makontena 349 wamefikishwa mbele ya mahakama ya Kisutu kujibu tuhuma za kuhujumu uchumi na kuisababishia serikali kukosa kodi kiasi cha bilioni 12.7.Washitakiwa hao akiwemo kamishina wa forodha Tiagi Masamaki walikosa dhamana na kurudishwa rumande.


Thursday, December 3, 2015

MAMBO 15 KATIKA HOTUBA YA MAGUFULI NA WAFANYABIASHARA(SEKTA BINAFSI) NI MATUMAINI MATUPU KWA WATANZANIA

Raisi Magufuli

Hakika hiki ndicho tulichokosa Watanzania kwa muda mrefu jana Mweshimiwa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania alipata wasaa wa kuzungumza kwa mara ya kwanza na baadhi au wajumbe(wawakilishi) wa wafanya biashara hapa Tanzania

Hotuba yote ilijaa msisimko wa hali ya juu huku akiaanisha maeneo ambayo watanzania walikuwa wakiyasema sana ila masikio ya viongozi waliopita walifumba macho na kuziba masikio kabisa kabisa mambo hayo ni

i.Usafirishaji wa mchanga kwenda nje nchi kusafishwa wakati hatua za kusafisha ni rahisi kabisa akisisitiza.

ii.India kuwa nchi ya kwanza kuuza Tanzanite na Kenya ya pili wakati inatoka Tanzania

iii.Nchi kushindwa kuwa na viwanda hata vya toothpick au vibiriti

iv.Wawekezaji kuviachaa viwanda ambavyo walinunua wakati wa ubinafsishaji

v.Ndege kutua maeneo ya migodi na kubeba visivyojulikana

vi.Tanzania kukosa viwanda vya ngozi wakati ni ya pili baada ya Ethiopia kwa Africa

Vii.Watanzania kuzodolewa kuwa hawawezi kuwekeza katika nchi yao kwa kuwa hawana mitaji na wawazawa watapewa kipaombele atakaye chelewesha atakiona.

viii.Uporaji wa ardhi kwa matajiri na kupewa hati katika maeneo ya wazi

ix.Kukosa kiwanda cha samaki hali tuna eneo kubwa la uvuvi

x.Kahawa kukosa soko kutokana na kodi,sukari,viwanda vya maziwa n.k

xi.Ukwepaji wa kodi kwa wafanyabiashara wakubwa,na matajiri kuwa mawakala wa walipa kodi wadogo kwa TRA.

xii.Sekta ya utalii ni changamoto ni kwani hatuja pata mapato ya kutosha.

xiii.Siku saba wafanyabiashara wakalipe kodi zao walikwepa.

xiv.Mabenki yawe na ubunifu kuliko kufanya biashara na serikali.

xv.Mashine za TRA kwa nini zisitolewe bure halafu 

MAJALIWA AFUMUA UOZO MWINGINE BANDARINI NA SHIRIKA LA RELI,PATA TAARIFA YOTE HAPA





WAZIRI
MKUU ATINGA TENA BANDARINI NA TRL


*Akuta makontena 2,431
yametoka bila kulipiwa ushuru


*Ataka majina yaletwe
ofisini leo saa 11 jioni


*Atoa wiki wiki moja
kwa mfumo wa malipo kubadilishwa


*Akagua mabehewa, awaweka
kiporo TRL





WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara
nyingine ya kushtukiza bandarini na kukagua mfumo wa upokeaji na utoaji mizigo
na utozaji wa malipo baada ya kupewa taarifa kwamba kuna makontena 2,431
yametolewa bila kulipiwa ushuru.Waziri Mkuu alisema kwa mujibu wa taarifa ya
ukaguzi wa bandari ya kuanzia Machi hadi Septemba 2014, makontena hayo yalipita
bila kulipiwa kodi kupitia bandari kavu nne (ICDs) ambazo ni JEFAG, DICD, PMM
na AZAM.Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ni watumishi 10
tu ambao wamesimamishwa kazi kutokana na makosa hayo. “Mmeamua kuwasimamisha
kazi watu wadogo na kuwaacha wakubwa wanaendelea na kazi. Hatuwezi kuendelea kuikosesha
Serikali mapato namna hii,” alisema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu amemtaka Kaimu Meneja wa
Bandari, Bw. Hebel Mhanga amletee ofisini majina ya watumishi wote waliohusika
na ukwepaji kodi huo ifikapo leo saa 11 jioni. Pia amempa Meneja huyo wiki moja
kuhakikisha kuwa mamlaka hiyo inabadilisha mfumo wa utozaji malipo kutoka kwenye
billing system na badala yake kuweka mfumo
wa malipo wa kielektroniki (e-payment).

Ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Desemba 3,
2015), wakati akikagua idara mbalimbali za mamlaka ya bandari na kuona ukaguzi
wa mizigo unavyofanyika kwa kutumia scanners. Akiwa kwenye chumba cha scanner mojawapo, Waziri Mkuu alikuta manifest moja ikisema kontena limejaa diapers lakini picha ya kwenye kompyuta ya
scanner ilionyesha kuwa ndani ya kontena
hilo kuna vitu kama vifaa vya umeme.


Kwa mujibu wa Kaimu Meneja Bandari upande wa
Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA), Bw. Ben Usaje ambaye pia ni msimamizi wa kitengo cha scanner, inapobainika taarifa kama hiyo
inapaswa itumwe kwa wenye ICDs ili wafanye ukaguzi kwa kulifungua kontena ili
kuhakikisha mali zilizomo ndizo zilizoandikishwa kwenye manifest.

Katika
hatua nyingine,
Waziri Mkuu Majaliwa amefanya ziara ya kushtukiza kwenye ofisi za Shirika la
Reli (TRL) na kukagua mabehewa yaliyokuwepo kisha akazungumza na baadhi ya wafanyakazi
waliokuwepo kwenye stesheni hiyo ambako alibaini madudu kwenye malipo ya
mishahara na makato ya michango ya wafanyakazi.

Akizungumza na Mkurugenzi Mkuu TRL, Mhandisi
Elias Mshana, Waziri Mkuu alisema amefika kwenye shirika hilo ili kujifunza
utendaji wao kazi lakini anazo taarifa za wao kupewa fedha na Serikali kiasi
cha sh. bilioni 13.5/- ili waendeleze miundombinu ya reli lakini hawakufanya
hivyo. “Nia ya kuwapa fedha hizo ilikuwa ni kuboresha miradi ili muweze
kujiendesha kibiashara lakini nyie mkaamua kujilipa wenyewe,” alisema.

“Ninazo taarifa kuwa baada ya hapo, mlikopa
sh. bilioni 3 kutoka benki ya TIB ili kuendesha miradi ya shirika lakini badala
ya kufanya miradi, fedha hizo mkaamua nazo kujilipa mishahara. Sasa sijui
mnarudishaje huo mkopo wakati hakuna mradi wowote uliofanyika,” alihoji bila
kupata majibu.

Alipoulizwa wafanyakazi wana matatizo gani
hapo TRL, Katibu wa TRAWU, Bw. Boaz Nyakeke alisema wanadai malimbikizo ya
makato yao kwenye mifuko ya pensheni, malimbikizo ya makato kwenye SACCOS na malimbikizo
ya kuanzia Julai – Novemba 2014.


Waziri Mkuu kwa upande wake alimtaka
Mhandisi Mshana asimamie uboreshaji huduma za usafiri wa treni katika Jiji la
Dar es Salaam ili hata mabasi ya mwendo kasi yatakapoanza wananchi waweze kuwa
na uhuru wa kuchagua aina ya usafiri wautakao.

“Tunataka kujenga yadi kubwa nje ya mji ili watu
wenye magari wawe wanayaacha huko na kutumia usafiri wa treni au DART kuja
mjini kama njia mojawapo ya kupunguza msongamano wa magari jijini Dar es
Salaam,” alisema.

Tuesday, December 1, 2015

TANZANIA:BEI YA PETROL NA DIZELI YASHUKA HUKU MAFUTA YA TAA IKIPANDA.

EWURA(Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji imetangaza punguzo la bei za kikomo kwa Petrol,Dizeli na Mafuta ya taa kuanzia Desemba 2.

Petrol imeshuka kwa asilimia 1.38 sawa na Shs 28

Dizeli ikishuka kwa asilimia 2.96 sawa na Shs 56

Mafuta ya taa yameongezeka kwa asilimia 1.85 sawa Shs 32.

Tokeo la picha la petrol station


ALIYEKUWA KAMISHINA WA TRA ATAJWA KUHUSIKA UPOTEVU WA DOLLA BILLIONI SITA.

Aliyekuwa Kamishina Mkuu Harry Kitillya katika sakata la sasa kuhusiana na pesa ambayo Tanzania ilikopa kwa ajili ya maendeleo ya nchi huku ikisaidiwa na Stanbic Bank kuezesha mkopo ambao umebainika kuwa kuna ongezeko la kama dola billioni sita ambazo zilipwa kwa kampuni ya EGMA.

EGMA ambayo iliundwa mwaka 2011 kama mshauri wa masuala ya uwekezaji hivyo katika wakati ambao makubaliano yakifanyika na pesa kupewa Tanzania Kitillya ndie aliyekuwa Mkurugenzi wa Bodi kabla ya kustaafu.Hivyo kati ya watu waliotajwa kuhusika katika dili hili Kamishina Mstaafu ametajwa na wengine ni Mboya(Marehemu) na Gasper Njuu.

Tokeo la picha la harry kitillya

Sunday, November 22, 2015

RAISI MAGUFULI KASI 180 KUPUNGUZA MATUMIZI YASIO NA TIJA TENA SERIKALINI

Baada ya Rais Magufuli kufuta utaratibu wa sherehe za wabunge na kuweka bajeti ndogo kabisa katika tafrija hiyo iliyokuwa itumbue zaidi milioni 235 na kuhamishia fedha zote katika kununu vitanda vya wagonjwa pale Muhimbili agizo ambalo limeshafanyiwa kazi na vitanda vimeshanunuliwa na vinaendelea kufungwa tayari kuwwapatia wagonjwa wanaolala chini.

Wakati huhuo Raisi amekata safari ya viongozi walitarajia kwenda kwenye mkutano wa Jumuiya ya Madola kwa taarifa safari hiyo ingeweza kuwa na gharama ya milioni 700 kama viongozi wote wangeenda na badala yake ni viongozi wanne walioruhusiwa kwenda.

Tokeo la picha la images of magufuli

Monday, October 19, 2015

FACEBOOK yalalamikiwa na watumiaji kuwa chanjo cha SMARTPHONE nyingi kuisha chaji.

Kampuni ya Facebook imeingia matatani baada ya watumiaji wake wengi kulalamikia kuwa IPHONE(SMARTPHONE)zimekuwa chanjo cha simu zao kuisha chaji haraka,kwaniwanalala hata ukizima simu Facebook application itakuwa inaeendelea kufanya kazi pasipo wewe kugundua.

Kupelekea hili kampuni imeamua kuchukua hatua na kufanya upembuzi yakinifu ili kugundua nini kinasababisha.Hivyo wameaahidi kulifanyia kazi ili kupata suluhisho na kuondoa kero hii kwa watumiaji wake.Kweli wezetu wanawajibika.

Tokeo la picha la facebook logo

Thursday, October 15, 2015

SOKO LA FEDHA ZA KIGENI KULINGANA NA BENKI KUU YA TANZANIA KWA LEO

Wednesday, October 14, 2015

UCHUMI SUPERMARKET YAFUNGA MADUKA YAKE TANZANIA ZAIDI YA AJIRA 400 ZAPOTEA

Dar es Salaam. Uongozi wa Uchumi Supermarket umetangaza kufunga shughuli zake katika maduka yake yaliyopo Tanzania na Uganda ili kutoa nafasi ya kuzuia mtikisiko wa kifedha unaoikumba kampuni hiyo. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Uchumi, Dk Julius Kipng'etich, amesema Bodi imeamua kufunga vitengo vya kikanda ili kuimarisha shughuli zake nchini Kenya baada ya kupata hasara katika maduka yake ya Uganda na Tanzania. "Maduka yetu ya Uganda na Tanzania huchangia asilimia 25 tu ya gharama za uendeshaji. Matawi hayo mawili hayajapata faida yoyote kwa zaidi ya miaka mitano iliyopita jambo linaloyumbisha shughuli zetu," amesema Dk Julius "Tuna uhakika kwamba tunaweza kuigeuza Uchumi kwa kulenga asilimia 95 ya biashara ambazo zinaleta fedha kwa wanahisa ambao wana matumaini kwamba tutafanikisha hili ndani ya muda mfupi," ameongeza Dk Kipng'etich. Kwa upande wa Tanzania, juzi wafanyakazi zaidi ya 400 waligoma kwa kujifungia ndani ya ofisi zao kwa zaidi ya saa 20 wakitaka kujua hatma yao kwenye makao makuu ya duka hilo yaliyopo katika jengo la Quality Center jijini Dar es salaam. Najaribu kutafakari kwa nini wawekezaji wengi wamekuwa wakishindwa kuwekeza vyema ni habari ya kusikitisha na hiyo imekuwa ikitokea mara kwa mara mfano mzuri mahoteli makubwa yamekuwa yakishindwa kwa miongo kadhaa kama Sheraton,Movenpick,kwa upande wa maduka makubwa Shoprite wamekwenda kwa sababu hizo hizo na kwenye utalii na migodi hali kadhalika.Kuna kitu kama nchi inapaswa kufanya hapa Hii si habari njema katika kipindi hichi ambacho vijana wengi wamekuwa wakitafuta ajira za kuajiria inabidi viongozi wetu wa serikali wajipange katika hili.

Tuesday, October 13, 2015

VIWANGO VYA SOKO LA KUBADILISHIA FEDHA LEO