Hakika UKAWA hawana budi kuendelea kuikosoa serikali ya Raisi John Pombe Magufuli kwani ndio kazi yao itakuwa kitu cha ajabu kwa chama cha upinzani kushabikia au kuridhika na mwenendo wa serikali kwani kazi yao kama chama cha upinzani itakuwa haina maaana.Kwa kufanya hivyo itaifanya serikali iliyo madaraki isibweteke ni vyema kuendelea kufanya hivyo ili serikali iweze kutambua mapungufu na kufanya marekebisho adri iwezekanavyo.Lakini wananchi tunapaswa kuwa makini katika kuchambua yapi mazuri kwani wanasiasa ni kama vinyonga leo kijani kesho blue.
0 comments:
Post a Comment