Wananchi wa Tanzania kwa takribani mwezi mzima wamepata taabu kubwa baada ya sukari kuadimika.Hii imekuja baada matamko ya serikali baada ya kutoa bei elekezi na kusitisha vibali vya uwagizaji bidhaa hii.Baadala ya kutafuta njia mbadala na zilizosahihi wafanya biashara wakaficha sukari wakidhani serikali ingerudi nyuma.Kibao kimewageukia na njama zao potofu hakika rai yangu serikali isimame imara na isirudi nyuma kwa hili,kuteseka huku ni kwa muda wananchi wa hali ya chini ndio waliokuwa na taabika siku zote natumai mipango ya serikali ikikaa vizuri kila mtu atafurahi na wale wanaopinga hatua hizi watakuja kubadilika tuu,mabadiliko yoyote si rahisi kukubalika mapema hivyo tunabudi ya kuyakubali na matunda yataonekana baadaye.
0 comments:
Post a Comment