Saturday, October 31, 2015

MATAMKO YA MAALIM SEIFU YAKEMEWA ZANZIBAR

Tokeo la picha la images of maalim seifu

Baada ya zoezi la uchaguzi kusitishwa na Tume ya uchaguzi ya Zanznibar.Kwa kipindi sasa kumekuwa na matamko mbali mbali kuelezea sintofahamu hiyo.Balozi za Marekani na Uingereza wakielezea mtizamo wao kuhusu suala la uchaguzi na kutoa matamko kuwa zoezi hilo halina budi kuendelea kwani si haki kwa wananchi wa Zanzibar kwani wanahitaji kupewa haki yao

Kwa upande mwingine baadhi ya viongozi wa Tume wametoa kauli zao kwa kusema kuwa uwamuzi huo wa kusitisha zoezi la kuesabu kura ni uamuzi wa mtu binafsi Mwenyekiti wao Ndugu Jecha na sio wa Tume hivyo wanamtaka afute kauli ili zoezi liendelee

Maalim Seifu mgombea kiti cha Uraisi kupitia CUF ametoa matako mbali mbali tangu kusitishwa kwa zoezi hilo,huku akitaka viongozi wa juu wa serikali ya Zanzibar na Jamuhuri kutoa matako kuhusu hatma ya uchaguzi huo,akieendelea na matamko yako amesema wametoa siku kwa jumuiya ya kimataifa na serikali ikishindikina basi wao wataweza kuamua kama chama nini cha kufanya.

Hata hivyo leo vingoziwa CCM walilani matamko ya Seifu wakisema kuwa yanaweza kuhatarisha amani ya visiwani humo kwa hiyo Ndugu Maalim Seifu hana budi kuachana na matamko ya jinsi hiyo hayo yamezungumza Vuai Nahodha.

Hivyo hakuna budi kwa serikali sasa kutoa tamko kuhusu sakata hili maana mengi yamezungumzwa hivyo kuna haja ya kulimaliza swala hili mapema kabla matatizo makubwa hayatokea. 

0 comments:

Post a Comment