Waziri Mkuu wa zamani Tony Blair ameshangaza dunia kwa kuomba msamaha na kukiri uvamizi wa Iraki haukuwa sahihi ni takribani miaka 12 imepita tangu uvamizi wa Iraki ufanyike na kipindi chote hicho Tony Blair hakuwahi kukiri kuwa haikuwa sasa kuipiga Iraki kivita.Ikikumbukwa George Bush na Tony Blair wao ndio waliokuwa wakishinikiza kuwa Iraki lazima ipigwe kivita kwa kuwa ina silaha za maangamizi enzi hinzo ikiwa chini ya utawala wa Saddam Hussein ambaye baadaye alinyongwa hadi kufa.Dunia ilipiga kelele lakini Tony alijitetea na kusema ilikuwa sahihi.Leo hii amekiri na kuomba msamaha haikuwa sahihi kwani walipewa taarifa ambazo sio na usalama na hii imepelekea kuundwa kwa kundi la kigaidi la ISIS ambalo linafanya unyama mkubwa.
Je Tony Blair ataweza kushitakiwa kama mwalifu wa kivita baada ya kukiri walifanya kosa kubwa kuipiga Iraki walipokubaliana na swaiba yake George W Bush.Afrika tumeshuhudia viongozi wengi wakivikishwa katika mahakama ya ICC kwa makosa ya kivita kama haya.
Tony Blair na George Bush
Tony Blair akiwa Basra na wanajeshi kipindi cha kuipiga IRAKI-2003
0 comments:
Post a Comment