Tuesday, December 22, 2015

UPENDO WA AJABU KWANI BINADAMU WOTE NI SAWA

Katika hali ya sasa ambako kila kona ya dunia tunashuhudia mashambulizi ya kigaidi mengine yakihusisha utengano wa dini kati ya ya Waislamu na Wakristo.Hivi karibuni nchini Kenya kulitokea utekaji wa basi na magaidi wa Alshabab kwa lengo la kuwaangamiza wakristo wote ambao walikuwa Abiria baada ya kuwatangazia kuwa abiria wakislamu wako salama.

Ndipo upendo na ubinadamu na ile dhana iliyojengwa kwa baadhi yetu kuwa waislamu ni wapenda machafuko ilipojizihirisha kuwa sio kweli ni mitazamo ya watu wabaya.Baada ya tangazo hilo baadhi ya wanawake wakislamu waliokuwa abiria ilibidi wavue hijab zao na kuwafunika wale wa dhehebu la kikristo ili kuwaepusha na maangamizi dhidi ya magaidi hawa wanaotia doa dini inayo huburi upendo ya uislamu na kuweza kuwaokoa na vifo.

Tukio hili ni la kuigwa sana kwani binadamu wote ni sawa licha ya tofauti zetu za rangi,dini lakini hakuna tunachotofautiana mbele ya mwenyezi Mungu.

0 comments:

Post a Comment