Hali ya ufisadi barani Africa imekuwa sugu kwa mataifa mengi viongozi wa serikalini wamekuwa wakituhumiwa katika kashfa mbali mbali za ufisadi.Nchi nyingi zimeonyesha nia ya kupambana na ufisadi ikiwemo Kenya,Nigeria na Tanzania huku hatua mahususi zikichukuliwa kukabiliana na ufisadi kama kuwafukuza kazi na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wale wote waliobainika na ufisadi.
Shirika la TRANSPARENCY INTERNATIONAL kwa mara kwanza imebainisha kuwa wafanyabiashara ndio MAFISADI wakubwa barani Afrika na maafisa wa polisi kuwa ni vinara.Wananchi wamekuwa wakihitajika kutoa hongo ili waweze kupata huduma muhimu jambo ambalo limekuwa chanzo cha umaskini mkubwa sana katika bara hili.
Nchi inayoongoza Afrika kwa sasa ni Liberia huku Cameroon,Nigeria na Siera Leone zikifuata.Nchi za Botswana,Mauritius na Cape Verde zikiwa na asilimia chache kabisa za ufisadi.Hili ni nyanga Afrika mikakati inahitajika kutokemeza hili.
Kataa Rushwa kwa nguvu zote.
0 comments:
Post a Comment