Hapa kazi tuu
Kumekuwa na vilio vya hapa na pale juu ya mwenendo mzima wa kipato cha mtu binafsi ndani ya nchi yetu katika kipindi hichi cha Raisi Magufuli huku wengi wakilalamika maisha ni magumu sana.Mara baada ya Raisi kuingia madarakani kipaombele chake kilikuwa ni kupunguza matumizi yasio ya lazima ndani ya serikali na badala yake fedha ziende kwenye matumizi yenye tija na kukusanya kodi.
Hatua hii ya serikali kutangaza vita hiyo inaonekana kuwa shuburi nzito katika maeneo mbali mbali kwa mfano,Baa ,Hoteli,Catering,Makampuni binafsi.Utafiti unaonyesha kuwa mapato yamepungua kwa kiasi kikubwa hasa na inaoneka hali hii inaweza kuwa tishio kwa ustawi ya sekta hizo.
Nini kinaweza tokea sasa upo uhakika kabisa baadhi ya waajiri kuamua kupunguza wafanyakazi na hivyo kuongeza tatizo la ajira ndani ya nchi.Hata wale ambao walikuwa wamejiari wanaweza kushindwa tena kwani kuna baadhi walitegemea semina na warsha za serikali ili wapate tenda.
Mimi binafsi naamini hali itakuwa sawa tuu hata kipindi cha Mkapa wananchi walipitia hali hii,ni ujinga kuendelea kutumbua hela za serikali na kunufaisha watu wachache kwa dili za semina na warsha zisijo na tija huku hali kwa mwananchi wa kawaida akikosa mahitaji muhimu.Magufuli aeendelee na kasi hii ili wananchi watambue heshima ya kufanya kazi zaidi kuliko kuamini katika njia za mkato zisizo na tija kwa taifa.
Hizo ni siku 70 tuu je ndani ya siku 1750 ya uongozi wake tutakimbia nchi?
0 comments:
Post a Comment