Mchezaji wa kimataifa kutoka Tanzania Mbwana Ally Samatta amefanikiwa kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza soka ndani ya Afrika.Hakika Samatta ameweza kuwa shujaa na mwanamapinduzi wa ukweli nje ya Tanzania haya ni mafanikio binafsi lakini kwa Taifa pia limepata faida kubwa.
Ni wakati sasa kwa wachezaji wengine kujiwekea malengo kuweza kuvuka record hii ya Samatta ambaye kwa habari za sasa anaacha na TP Mazembe ili kwenda Ulaya kama dili zake zitafanikiwa.Na hivyo anaweza kuja kukaa tena meza moja kugombea zawadi ya kuwa mchezaji bora nje ya Afrika kama tulivyo ona kina Toure,Etoo n.k.Na hakika kwa matazamo wa Samatta atafanikiwa.
0 comments:
Post a Comment