Didier Drogba foundation imeingia katika kashfa nzito za matumizi yasiyoeleweka kwa hela ambazo zilichangwa kwa makusudi ya kutengeneza hospitali ya kisasa katika jiji la Abijan lengo ni kusaidia watu wenye matatizo mbalimbali ya afya.Vyanzo vinasema ni hela takriban Pound 1.7 milioni zilichangwa na watu maarufu wachezaji mbali mbali wa Chelsea John Terry,Cole,Lampard na wengine kama David Beckham lakini hadi sasa ni Pound 14,115 tu ndio zilizotumika...