Friday, September 2, 2016

SIKIA HII YA RAISI WA TANZANIA JOHN POMBE MAGUFULI

Katika hali ambayo haikutarajiwa Raisi amewesahii wale wote ambao wameficha mapesa wakiogopa wanaweza kugundulika baada ya kuzipata kwa njia ambazo sio halali hasa kwa msemo wa mjini KUPIGA DILI wameaswa wazitoe ziingie kwenye mzuko.Kwani kwa mamlaka aliyonayo anaweza amuru kuchapisha fedha mpya mara moja ili aweze kuwazibiti wenye fedha hizo haramu.

Tokeo la picha la picha ya noti ya elfu kumi

Wednesday, June 29, 2016

YANGA HOI MBELE YA TP MAZEMBE

Licha ya kuonyesha kandanda safi katika kipindi cha kwanza timu ya Dar Young Africans ilishindwa kupata matokeo na kuruhusu goli katika kipindi cha pili.Kipigo hicho ni cha pili kwa Yanga hivyo kuifanya kushika mkia katika kundi.Bope ndio alikwamisha bao ktk dk 73.

Tokeo la picha la picha ya yanga na tp mazembe

Thursday, May 12, 2016

UKAWA UKOSOAJI JUU YA MWENENDO WA SERIKALI UENDELEEE

Hakika UKAWA hawana budi kuendelea kuikosoa serikali ya  Raisi John Pombe Magufuli kwani ndio kazi yao itakuwa kitu cha ajabu kwa chama cha upinzani kushabikia au kuridhika na mwenendo wa serikali kwani kazi yao kama chama cha upinzani itakuwa haina maaana.Kwa kufanya hivyo itaifanya serikali iliyo madaraki isibweteke ni vyema kuendelea kufanya hivyo ili serikali iweze kutambua mapungufu na kufanya marekebisho adri iwezekanavyo.Lakini wananchi tunapaswa kuwa makini katika kuchambua yapi mazuri kwani wanasiasa ni kama vinyonga leo kijani kesho blue.

Tokeo la picha la ukawa bendera

Monday, May 9, 2016

HUJUMA HIZI SI ZA KUZIACHIA HATA KIDOGO

Wananchi wa Tanzania kwa takribani mwezi mzima wamepata taabu kubwa baada ya sukari kuadimika.Hii imekuja baada matamko ya serikali baada ya kutoa bei elekezi na kusitisha vibali vya uwagizaji bidhaa hii.Baadala ya kutafuta njia mbadala na zilizosahihi wafanya biashara wakaficha sukari wakidhani serikali ingerudi nyuma.Kibao kimewageukia na njama zao potofu hakika rai yangu serikali isimame imara na isirudi nyuma kwa hili,kuteseka huku ni kwa muda wananchi wa hali ya chini ndio waliokuwa na taabika siku zote natumai mipango ya serikali ikikaa vizuri kila mtu atafurahi na wale wanaopinga hatua hizi watakuja kubadilika tuu,mabadiliko yoyote si rahisi kukubalika mapema hivyo tunabudi ya kuyakubali na matunda yataonekana baadaye.

Tokeo la picha la sugar tonnes

TODAY'S MESSAGE

The best way to motivate yourself is to stop stressing about what'll happen when things go wrong and start thinking about how awesome life will be when they go right.

Tokeo la picha la laughing images of african

Friday, April 15, 2016

DIDIER DROGBA NDANI YA TUHUMA YA UFISADI KUPITIA MFUKO WAKE

Didier Drogba foundation imeingia katika kashfa nzito za matumizi yasiyoeleweka kwa hela ambazo zilichangwa kwa makusudi ya kutengeneza hospitali ya kisasa katika jiji la Abijan lengo ni kusaidia watu wenye matatizo mbalimbali ya afya.Vyanzo vinasema ni hela takriban Pound 1.7 milioni zilichangwa na watu maarufu  wachezaji mbali mbali wa Chelsea John Terry,Cole,Lampard na wengine kama David Beckham lakini hadi sasa ni Pound 14,115 tu ndio zilizotumika huku ikionekana mradi uliokusudiwa ukiwa unasusua.

Hii ni tuhuma nzito sana kwa Didier kama atashindwa kutetea matumizi ya fedha zilizochangwa kwani kuputia mfuko huu ameweza kupata fursa nyingi kama kuwa balozi wa UN na Pepsi lakini matokeo yake ameshindwa kutikiza ndoto ya kusaidia watu maskini ni swala linalofanyiwa uchunguzi mambo yakiisha itajulikana mbivu na mbichi.

Tokeo la picha la didier drogba foundation

Tuesday, March 1, 2016

WALIMU KUFUTIWA NAULI DAR NI MOJA YA HATUA YA KUBORESHA AU CHANGAMOTO MPYA

Kuanazia leo lile tamko la Mkuu wa wilaya Bwana Makonda kuwa walimu katika wilaya Kinondoni wataweza kupanda mabasi bure kuanzia saa kumi na moja mpaka saa mbili na saa tisa mpaka kumi na moja jioni.Wengi wametoa maoni yao kuwa ni hatua nzuri katika kuboresha na kujali taaluma hii ambayo bado haina kipao mbele kikubwa katika nchi yetu licha ya kuwa ni nguzo muhimu katika maendeleo ya nchi yoyote duniani.Kwa miaka mingi kumekuwa na vilio juu ya maslahi yao ila mambo bado ni magumu sana.Tumaini langu kuwa kama huyu ameweza kuona hili itafika siku yataonwa na mengine lengo nikuweza kubadilisha hali ya walimu wetu.
Licha mtazamo huo wengine wamebeza na kusema hicho ni kitu kidogo sana kwani walimu wanayo matatizo zaidi ya hayo ni kweli na yanajulikana.Je tukiacha hayo nionavyo mimi inaweza ikawa changamoto mpya hasa kama kwa Makonda wa mabasi hao kuwa chanjo cha kuwatenga na kuwasema vibaya wale ambao tumezoea usafiri huu tunajua Makonda walivyo na maneno ya kashfa na jambo hili jema likwa shuburi licha la kupitishwa na wamiliki wao.Wito yapashwa elimu juu ya hili itolewe vizuri ili lisije likaeleweka vibay na kuwazalilisha walimu wetu wanaofanya kazi nzito na isihishie kuwa amri tu.Natumaini ipo siku walimu wataona faraja na kuthaminiwa zaidi.
Tokeo la picha la teachers in Tanzania photo

Monday, February 8, 2016

Hili la Zanzibar linahitaji hekima ya juu lifikie mwafaka

Hali ikiwa bado si shwari sana visiwani Zanzibar huku tarehe ya uchaguzi ikiwa imeshatolewa na Tume ya Uchaguzi.CUF wakitoa tamko la kutoshiriki uchaguzi huo bado ni tamko tete hasa hasa.Huku baadhi wanasheria wakitoa mitazamo hayo juu ya hii.

Jambo la msingi ni kupata hekima na busara  baina ya pande zote zinazosuguana kwani haki isipotendeka lolote baya laweza tokea.Haya yote kwa maono yangu yatafikia tamati kama sheria    itaingilia kati katika kupata haki kati ya hizi pande mbili ili mgogoro huu unaoendelea uweze kupita salama.

Tokeo la picha la zanzibar view

Arsenal hawako tayari kiakili kushinda taji la Uingereza-Thiery Henry

Nguli wa Arsenal Thiery Henry anapata wasiwasi juu ya mwenendo wa timu yake ya zamani kama kweli ipo imara kifikra katika kugombea kombe la ligi kuu ya Uingereza.Mwenendo wa Arsenal umekuwa wa kususua na kupata matokeo yasiyo na uhakika.Hii inamsikitisha kwani anaona Leicester wana nguvu kifikra katika kutaka kuchukua kombe ila kwa Arsenal kuna walakini kidogo.Tuone katika mechi zijazo nini kitatokea.

Tokeo la picha la thierry henry arsenal pundit

Tuesday, January 26, 2016

JE WAJUA ADEBAYOR KALA SHAVU CRYSTAL PLACE

Emmanuel Adebayor raia wa Togo hatimaye amepata timu tena baada ya kukaa kwa kipindi kirefu maana ya kuachana na Tottenham.Sasa ni mali ya Crystal Palace.Hii ni baada ya Alan Pardew (Kocha)kudhibitisha hilo kuwa anamuhitaji Emma katika timu hiyo.

Emmanuel Adebayor

Sunday, January 24, 2016

ARSENAL KURUDI KILELENI LEO DHIDI YA CHELSEA

Asernal inaweza kurudi kileleni itakapo kutana na Chelsea kwenye dimba la Emirates.Arsenal ambayo inatabiriwa kuwa inaweza kubeba kombe msimu huu baada ya kulikosa kwa zaidi ya miaka 10.Mechi inatarajiwa kuanza saa moja kwa majira ya Afrika Mashariki.

kTokeo la picha la chelsea vs arseanl logoKikosi cha Arsenal-(P.Cech,P Mate,L KoScielny,N Monreal,H Berlin,M Ozil,A Ramsey,A Sanchez,M Flamini,J Campell,O Giroud

Chelsea:T Courtois,B Ivanovic,K Zouma,J Terry,C Azpilicueta,C Febregas,J Obi,P Rodriguez,N Matic,Willian,D Costa.

Saturday, January 23, 2016

MAN U CHALII,LIVERPOOL BALAA,LEICESTER KILELENI TENA

Man united imefungwa goli moja na Southamphton,Liverpool imeipiga Norwich City 5-4 katika mechi tamu Lallan ndio alikuwa kinara baada ya kuifungia goli la tano.Leicester imerudi kileleni baada ya kuifinguka Stoke City 3-0.Watford imeifunga Newscastle 2-1.Tottenham imeifunga Crystal Palace 3-1.AFC Bournemouth na Sunderland 1-1 na Aston Villa na WBA.

C.RONALDO MARUFUKU KWENDA MOROCCO KUMTEMBELEA MSHIKAJI WAKE

C.Ronaldo amepigwa marufuku na Raisi wa Real Madrid F.Perez  kwenda Morocco kumtembelea rafiki yake Badr Hari.Perez amekwenda mbali anaweza kuomba wa Mfalme wa Morocco na rafiki Mohamed VI ili kumjulisha kama Ronaldo atakwenda huko.

Kitendo hicho cha C Ronaldo kwenda morocco kilishuhudia kiwango chake kushuka sana katika kipindi kifupi.

Cristiano Ronaldo and Badr Hari