Monday, February 8, 2016

Hili la Zanzibar linahitaji hekima ya juu lifikie mwafaka

Hali ikiwa bado si shwari sana visiwani Zanzibar huku tarehe ya uchaguzi ikiwa imeshatolewa na Tume ya Uchaguzi.CUF wakitoa tamko la kutoshiriki uchaguzi huo bado ni tamko tete hasa hasa.Huku baadhi wanasheria wakitoa mitazamo hayo juu ya hii.

Jambo la msingi ni kupata hekima na busara  baina ya pande zote zinazosuguana kwani haki isipotendeka lolote baya laweza tokea.Haya yote kwa maono yangu yatafikia tamati kama sheria    itaingilia kati katika kupata haki kati ya hizi pande mbili ili mgogoro huu unaoendelea uweze kupita salama.

Tokeo la picha la zanzibar view

Arsenal hawako tayari kiakili kushinda taji la Uingereza-Thiery Henry

Nguli wa Arsenal Thiery Henry anapata wasiwasi juu ya mwenendo wa timu yake ya zamani kama kweli ipo imara kifikra katika kugombea kombe la ligi kuu ya Uingereza.Mwenendo wa Arsenal umekuwa wa kususua na kupata matokeo yasiyo na uhakika.Hii inamsikitisha kwani anaona Leicester wana nguvu kifikra katika kutaka kuchukua kombe ila kwa Arsenal kuna walakini kidogo.Tuone katika mechi zijazo nini kitatokea.

Tokeo la picha la thierry henry arsenal pundit