Wednesday, September 30, 2015

Azam,Simba na Yanga mbele kwa mbele VPL

Kwa hakika ligi ya VPL msimu wa 2015/2016 ni raha tu,imekuwa na msisimko wa juu huku timu nne Yanga,Azam,Simba na Mtibwa zikiwa katika viwango vya juu.Azam,Simba,Yanga jana zilitoa dozi na kujiongezea point kuelekea katika kunyakuwa ubingwa wa VPL 2015/2016.Matokea ya jana yalikuwa YANGA 2 MTIBWA 0 -UWANJA JAMUHURI MOROGORO SIMBA 1 STANDA UNITED 0 -UWANJA WA TAIFA AZAM 2 COASTAL UNION 0 -UWANJA CHAMAZI COMPLEX

Utambue ugonjwa wa kipindupindu (cholera)dalili zake,maambukizi,kinga na tiba

Kipindupindu Ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria aina Vibrio cholera. Ugonjwa huu ni moja ya magonjwa ya nayoiathiri jamii hasa pale unapotokea kwani ni miongoni mwa magonjwa ya milipuko. Ugonjwa huu uambukizwa kutokana na vimelea vinavyopendelea kuishi kwenye kinyesi cha binadamu. Mtu anaweza kuambukizwa ugonjwa kwa kunywa maji au kula chakula kilichochafuliwa na kinyesi chenye vimelea vya kipindupindu. Baada ya mtu kula chakula au kunywa kinywaji chenye vimelea vya kipindupindu, baadhi ya vimelea huuawa kwa tindikali iliyopo kwenye utumbo pindi chakula au maji hayo yanapoingia tumboni. Hata hivyo baadhi ya vimelea hufanikiwa kukwepa tindikali hiyo na kuendelea kuishi. Vimelea hivyo vilivyofanikiwa kukwepa tindikali hiyo hujishikisha kwenda kwenye ukuta wa utumbo mdogo kwa kutumia maumbo maalum yaliyomo kwenye mwili wa binadamu ambayo huwezesha kusafiri ambayo kwa kitaalamu huitwa flagella. Vimelea hivyo viwapo kwenye utumbo mdogo hutoa sumu iitwayo CTX au CT(cholera toxin) ambapo sumu hiyo husababisha mtu kuhara choo chenye majimaji. Licha ya kutoa sumu hiyo pia huendelea kutoa kizazi kingine cha vimelea hao nje kwa njia ya haja kubwa. Iwapo choo hicho cha mtu aliyeambukizwa kipindupindu kitachanganyika na chanzo chochote cha maji au chakula watu wengine huweza kuambukizwa kipindupindu. Maambukizi yake Kipindupindu husababishwa na bakteria aina ya Vibrio cholerae zinazosababisha kuhara majimaji yenye rangi kama maji ya mchele. Kipindupindu hutokea hasa pale mazingira yanapokuwa sio safi kwa kiasi kikubwa kwani maji, vyakula, hata vyoo huweza kuwa katika hali ya uchafu. Bakteria ya vibrio cholerae hupatikana hasa katika kinyesi na maji ya choo na pia katika maji ya bahari, maziwa na mito kama maji machafu huingizwa katika magimba ya maji bila kusafishwa kwanza. Katika mazingira yenye maji ya bomba, yaliyosafishwa na karakana ya kusafisha maji machafu, kipindupindu hutokea mara chache sana. Dalili zake Dalili za awali za kipindupindu ni pamoja na kuhara ghafla choo chenye majimaji (kinakuwa na maji kama ya maji ya mchele) na choo hicho muda mwingine huwa na harufu kali kama shombo ya samaki. Kutapika .Pia mgonjwa huonyesha dalili za kupungukiwa na maji mwilini kama vile ngozi kuwa kavu, midomo kukauka, mgonjwa kuhisi kiu kikali, kupata mkojo kidogo sana. Pia mgonjwa huwa na homa kali. Kuishiwa nguvu na kujisikia mchovu sana pamoja na macho kutumbukia ndani hasa kwa watoto. Jinsi ya kutambua ugonjwa huu Ugonjwa huu huweza kugunduliwa na kutambuliwa kwa kuona dalili zake. Hata hivyo ili kudhibitisha kuwa kama dalili alizonazo mgonjwa zinatokana na ugonjwa huo vipimo vifuatavyo huweza kutumika kuwa na uhakika zaidi. Mgonjwa huweza kupimwa damu kwa hajili ya kuotesha vimelea vya kipindupindu katika maabara. Pia choo cha mgonjwa huweza kuchunguzwa kwa kutumia darubini(dark field microscope) ambapo kama ugonjwa ni wenyewe vimelea huweza kuonekana. Tiba Mgonjwa wa kipindupindu huweza kupatiwa matibabu huku lengo kuu likiwa ni kurejesha maji na madini mwilini aliyoyatoa kwa njia ya kuhara au kutapika. Njia itumikayo kumpatia maji hayo ni kwanjia ya mdomo ambapo hupewa anywe au kwanjia ya mshipa wa damu ambayo kitaalamu hujulikana kama intravenously(i.v) Mgonjwa hunyweshwa maji mengi, kwa sababu mwili wake hupoteza maji mengi anapougua maradhi haya kwa njia ya kuhara na kutapika. Dawa zinazojulikana kufanya kazi ni kama cotrimoxazole, erythromycin, doxycycline, chloramphenicol, na furazolidone. Jinsi ya kujikinga na kipindupindu Miongoni mwa njia zinazoweza kusaidia kuepuka na kupatwa na ugonjwa huu ni pamoja na upatikanaji wa maji safi na salama.Watu wengi wanatakiwa kuhakikisha wanapata maji safi na salama huku kabla ya kunywa maji hayo wanahakikisha wameyachemsha na kuyachuja pamoja na kuyahifadhi kwenye chombo safi. Ni muhimu kunawa mikono kwa maji safi na sabuni kila mara baada ya kutoka chooni ili kuepuka kula au kushika chakula chochote huku mikono ikiwa michafu. Pia jamii inashauriwa kufunika chakula kikiwa mezani ili nzi wasiweze kutua juu yake Licha ya kuzingatia usafi pia inashauliwa kujenga choo angalau mita 30 kutoka kilipo chanzo cha maji pamoja na kuweka mazingira katika hali ya usafi kwa ujumla. Ili kuweza kuepuka ugonjwa jamii inatakiwa kuzingatia usafi ikiwa ni pamoja na kunawa mikono kwa maji safi na salama kwa kutumia sabuni. Hii ni muhimu sana hasa kwa watoto wanapokuwa shuleni ili kuepuka kupatwa na ugonjwa huo. Pia ni muhimu kunawa kabla ya kuandaa chakula au kula huku ukizingatia usafi wa vyombo vinavyotumika kuandalia chakula au kulia chakula hicho. Kusafisha matunda kwa maji safi na salama hasa ya uvuguvugu kabla ya kuyamenya au kuyala kwa yale yasiyohitaji kumenywa. Kufunika chakula ili kuepusha uwezekano wa wadudu hasa nzi kutua juu ya chakula hicho kwani wanaweza kuacha baktelia wanaoweza kuwa wamewabeba kwenye miguu yao. Maji ya choo yanayotokana na wagonjwa wa kipindupindu yanapasa kupitia mashimo ya choo yaliyohifadhiwa vizuri ili kuzuia usambazaji wa bakteria Vifaa vyote vinavyotumiwa na wagonjwa vinapaswa kuchemshwa kwa maji ya moto Mikono inayoshika wagonjwa au nguo zao inapaswa kusafishwa kwa maji na sabuni Mashimo ya choo yanapaswa kutiwa dawa za kuua bakteria kwa kutumia klorini
Cholera -Bacteria-Vibrio cholerae Scanning electron microscope image of Vibrio.

Diamond kama kawa 2015

Mwanamuki Diamond ametajwa tena kuania tuzo za Headies za nchini Nigeria katika kipengele cha African Artiste,watanzania yetu ni support.

SIASA HATARI!!!! ALBINO WAKIMBIA MPAKA WA TANZANIA KUHOFIA IMANI ZA KISHIRIKINA

Katika hali ya kusikitisha albino waishio mpakani mwa Tanzania na Kenya wamelazimika kukimbilia Kenya kuhofia kutumia kama chambo na wanasiasa wa Tanzania katika kipindi hichi cha uchaguzi ili kuweza kushinda katika nafasi zinazotarajiwa kupigiwa kura 25-10-2015.Huku ikikadiriwa zaidi ya albino 35 kuwa wamekimbia na hii imekuja baada ya Mr Encok(albino)kushambulia na watu na kuacha na majeraha.Tatizo hili limekuwa lina shamiri sana toka 2000 mpaka sasa zaidi ya 75 wameshauwa kwa imani hii licha ya asasi nyingi kutoa elimu kuhusu albinism watu wameeendelea kuwa wakatili huku wakiamini watafanikiwa katika mambo kama watatumia viungo vya albino.Ni wakati sasa wakuwajali ndugu zetu na kuwalinda wito kwa serikali ichukue hatua kali kwa wote wanaojihusisha na imani hii potofu hasa waganga wanao toa msharti ya kupatiwa viungo vya albino.

Rais Kikwete kuwa mgeni rasmi onesho la Swahili International Expo.

Rais Kikwete anatarajia kuzindua onesho la utalii la Swahili International Expo ambalo linatalajiwa kuanza Oct Mosi hadi 3 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani city.Onesho hili linakuwa ni la pili baada ya lile la eawali kufanyika mwaka jana 1-4-2014 na liliweza kuvuta waonyeshaji 40 na mawakala 19 wa utalii(Hosted buyers).Jumla ya wageni 1200 waliweza kuhudhuria huku mdhamini mkuu akiwa Ethiopian Airline. Onesho la mwaka huu linatarajiwa kuwa na waonyeshaji takriban 100 huku wageni wanatarajiwa kuongeza kufika 2000.Bidhaa mbalimbali zitaonyeshwa kama,Tingatinga,Wachongaji vinyago,Vikundi vya burudani muziki(utalii bend),kikundi cha utamaduni kutoka chuo cha Tumaini(Arusha) Tanzania Tourist Board(TTB) imetoa wito kwa watanzania kuwa ma mwako mkubwa kwa mawak huu kutembelea maonyesho hayo kama njia nzuri ya kutambua na kujifunza mambo mengi kwani wadau wa utalii wenye uzoefu watakuwepo.

Tuesday, September 29, 2015

Asernal yafa tena UEFA yapigwa 3-2 na Olympiakos


Matumani ya Asernal kufika hatua ya mtoano yamefifia baada ya kufungwa tena na Olympiakos katika dimba la Emirates.Iliwachukua wageni dakika 33 kupata bao la kwanza kupitia kwa Felipe Pardo kabla ya Theo Walcott kusawazisha dakika ya 35 na dakika ya 40 David Ospina alijifunga mwenyewe.Alexis Sanchez mnamo dakika 65 aliisawazishia tena Asernal lakini kama vile bahati haikuwa kwao tena dakika moja baadae Aflred Finnbogason akahitimisha msiba mwingine na kufunga bao la tatu.Kwa matokeo hayo Asernal wako katika hali mbaya kwani wanaisubilia Bayern Munich ambayo ilipata matokea mazuri kwa kuifunga Dinamo Zagreb 5-0.

FAHAMU UGONJWA WA BAWASIRI AU KUOTA KINYAMA SEHEMU YA HAJA KUBWA NA NAMNA YA KUEPUKA NA UGONJWA HUU

NA JAMIIMOJABLOG)

WATU wengi wanasumbuliwa na tatizo hili ambalo huwafanya kuwa na uoga na aibu wa kuelezea na kushindwa hata kwenda hospital kupata tiba

JE, UNAJUA BAWASIRI/HEMORRHOIDS NI NINI????!!
~Ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani na Inje ya sehemu ya haja kubwa na wakati mwingine mishipa hiyo huweza kupasuka/kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kasababisha kutoka kinyama au uvimbe.

~ugonjwa huu wa bawasiri kwa lugha ya kitaalamu tunauita HEMORRHOIDS ilhali kwa lugha ya kingereza unafahamika kama piles
~tatizo hili huwaathiri watu wote ila zaidi huwaathiri watu wazima kuliko watoto na inakadiriwa kuwa karibu 50%ya watu wote wako katika hatari ya kupata tatizo hili katika umri wa miaka 30_50


AINA ZA BAWASIRI

~Kuna Aina mbili za bawasiri

(A) BAWASIRI YA NDANI
~Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa huwa haiambatani na maumivu na wengi huwa hawajitambui kuwa Wana tatizo hili
~Aina hii hutokana na kuvimba na kuharibika kwa mshipa wa artery za ndani ya mfereji wa haja kubwa
~Aina hii imegawanyika katika madaraja manne
(1)DARAJA LA KWANZA ~Hii ni bawasiri ambayo haitoki mahali pale panapohusika
(2)DARAJA LA PILI ~hii hutokea wakati wa haja na kurudi yenyewe ndani baada ya kujisaidia.
(3)DARAJA LA TATU :hii hutokea wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kurudisha ndani yeye mwenywe.
(4)DARAJA LA NNE :hii ni bawasiri inayotoka na huwa ngumu kurudi

(B)BAWASIRI YA NNJE
~Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa na huambatana na maumivu makali na kuwashwa kwa ngozi katika eneo la tundu Hilo pia husababisha mishipa ya damu (vena) kupasuka na damu kuganda na kasababisha Aina ya bawasiri iitwayo THROMBOSED HEMORRHOIDS


CHANZO CHA TATIZO

~chanzo halisi cha ugonjwa huu hakijapatikana ila Kuna vitu ambavyo huwa chanzo cha kupata ugonjwa wa bawasiri ambayo ni ÷
��KUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE
��KUHARISHA KWA MUDA MREFU
��TATIZO LA KUTOPATA CHOO
��MATATIZO YA UMRI
��KUKAA KITAKO KWA MUDA MREFU
��UZITO KUPITA KIASI
��MATUMIZI YA VYOO VYA KUKAA KWA MUDA MREFU
DALILI ZA BAWASIRI
��Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
��kupata maumivu makali wakati wa kujisaidia
��kutokea uvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
��kujitokeza kwa kinyama katika eneo la tundu Hilo
��kinyesi kuwa na damu na kunuka harufu mbaya sana


MATIBABU NA JINSI YA KUEPUKA TATIZO LA BAWASIRI

~matibabu ya bawasiri hutegemea na Aina ya bawasiri pia tiba iliyozoeleka ni kukatwa kinyama na kuendelea na lishe ya chakula hata hvyo tiba hii si nzuri kwasababu huwa haitibu chanzo cha tatizo hivyo huwa rahisi kujirudia hivyo tiba nzuri ni kutumia dawa na anion chip kubandika mahali penye tatizo na kuondoa tatizo Hilo

~Pamoja na hayo bawasiri ni ugonjwa unaoweza kuepukika kwa kuzingatia
��KULA MBOGAMBOGA ZA MAJANI, MATUNDA, NA NAFAKA ZISIZOKOBOLEWA
��KUNYWA MAJI MENGI ANGALAU GRASS 6/12 Kwa siku
��EPUKA KUKAA CHOONI KWA MUDA MREFU


MADHARA YA TATIZO LA BAWASIRI

��kupata upungufu wa damu (anemia)
��Kupata tatizo la kutokuweza kuhimil choo
��hupunguza nguvu za kiume na kuondoa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake
��kuathirika kisaikolojia
��kukosa moral ya kufanya Kazi kutokana na maumivu makali

WASILIANA KWA 0717035770 AU 0753692612.