Friday, April 15, 2016

DIDIER DROGBA NDANI YA TUHUMA YA UFISADI KUPITIA MFUKO WAKE

Didier Drogba foundation imeingia katika kashfa nzito za matumizi yasiyoeleweka kwa hela ambazo zilichangwa kwa makusudi ya kutengeneza hospitali ya kisasa katika jiji la Abijan lengo ni kusaidia watu wenye matatizo mbalimbali ya afya.Vyanzo vinasema ni hela takriban Pound 1.7 milioni zilichangwa na watu maarufu  wachezaji mbali mbali wa Chelsea John Terry,Cole,Lampard na wengine kama David Beckham lakini hadi sasa ni Pound 14,115 tu ndio zilizotumika huku ikionekana mradi uliokusudiwa ukiwa unasusua.

Hii ni tuhuma nzito sana kwa Didier kama atashindwa kutetea matumizi ya fedha zilizochangwa kwani kuputia mfuko huu ameweza kupata fursa nyingi kama kuwa balozi wa UN na Pepsi lakini matokeo yake ameshindwa kutikiza ndoto ya kusaidia watu maskini ni swala linalofanyiwa uchunguzi mambo yakiisha itajulikana mbivu na mbichi.

Tokeo la picha la didier drogba foundation