Thursday, November 26, 2015

AIBU AIBU AIBU SOKA TANZANIA

Tokeo la picha la images of tanzania soka



Mipango madhubuti ndio itakayo ikomboa Tanzania kuwa kichwa cha mwendawazimu katika soka.Kumekuwa na mipango isiyo na tija kwa muda mrefu hasa ndani ya chama cha mpira cha Tanzania.Unaweza sema mipango inayofanywa ki kwa ajili ya maslahi ya viongozi na sio katika soka.

Kamati ya ushindi ya TFF iliundwa kwa mbwembwe wengi tukatoa pongezi lakini matokeo yake imevunjwa baada ya kutolewa na Algeria sasa kama ilikuwa kwa mechi moja kuna haja ya kuwa na kamati kama hizi hazina tija kwani inasemekana imeacha deni la takribani milioni 70.

Watanzania wanapenda soka ila viongozi wamekosa mbinu na mikakati dhabiti katika kufanikisha hili.Maandalizi yao yamekuwa ya muda mfupi na yasioyo na dira.Naamini ndani ya Taifa la Tanzania lenye watu milioni 45 na ushee kupata vipaji vya watu 22 kuwakilisha Tanzania katika soka sio ndoto bali mipango hakuna.Tatizo nahisi watu wanatumia ofisi hizi kuendeleza CV zao na kupata maslahi binafsi na si kwa Taifa.Mara ya mwisho Tanzania imeshikiri katika mashindano ya mataifa katika miaka ya themanini kwa mara ya mwisho ni aibu kwa takribani miaka 35 hatuja fanikiwa tatizo liko wapi.

TFF anzeni kuwa na mipango ya dhabiti tuweze kuona mafanikio ya soka katika nchi yetu na sio ubabaishaji wa sasa.

0 comments:

Post a Comment