Monday, November 23, 2015

KAMA WABUNGE WANAMITAZAMO HII TUMEKWISHA

Kumekuwa na hali ya mpasuko kati ya wabunge walioteuliwa na wananchi juu ya maslahi yao.Kama ilivyo zoeleka katika awamu ya tatu na nne wabunge wamekuwa wakilipwa hela kwa ajili kununulia mashangingi(TOYOTA LAND CRUISER).Inasemekana wabunge wamegoma posho iliyopangwa kwa magari hayo kiasi cha milioni 90 kwa kila mmoja wangine wakitoa hoja shilingi la imeshuka thamani hivyo wanapaswa kupewa milioni 130 ili waweze kununua hayo magari.

Kwa nchi maskini kama Tanzania viwango staiki ambazo wabunge wamekuwa wakilipwa ni mzigo mkubwa kwa Taifa na naweza kusema ni mdudu mbaya sana kwa maendeleo ya Taifa letu.Kuna takribani wabunge zaidi ya 350.Staiki wanazozipata  kwa maoni yangu ni nyingi kwa Taifa kama maskini kama Tanzania na kama ningepata fursa ya kuongea na rahisi maoni yangu ningesema zipunguzwe.Na ikitokea hivyo naamini vita hii itakosa msuluhishi.Nasita kunuu kauli ya Raisi Magufuli msema kweli mpenzi wa mungu wabunge waache kupigania maslahi yao watanzania tuna shida nyingi ambazo zinahitaji maarifa na uweledi wao sio tamaa za utajiri na kujilimbikizia mali katika miaka watakayo kaa bungeni.

Hivyo wanapaswa kumuweka Mungu mbele na kuonyesha uzalendo wakupunguza matumizi yasio ya lazima milioni 130 kwa mahitaji ya jamii zingetosha kuleta zahanati,shule n.k.Ombi langu waweke uzalendo mbele kwa maendeleo ya Taifa kabla wananchi kuanza kuwashangaaa.

Tokeo la picha la landcruiser v8

Tokeo la picha la landcruiser v8


Tokeo la picha la landcruiser v8

Hii ndio V8 Wabunge wanazozitaka hakika ni anasa ambayo haiendani za maisha halisi ya Mtanzania.Nia aibu Muhimbili inakosa vitanda wao wanapigania V8 huku wapiga kura wao wakisota kwa maisha duni.

0 comments:

Post a Comment