Jana ilikuwa siku kubwa nchini Tanzania pale Mh John Magufuli alipoapishwa kuwa Raisi wa Tano wa Tanzania.Mamia ya wananchi walijitokeza kushuhudia hafla hiyo huku viongozi kutoka nchi mbali mbali za kiafrika na mabalozi walikuwepo pia.
Ni hatua muhimu kwa Taifa dogo la Tanzania lenye changamoto nyingi katika nyanja mbalimbali.Nasema ni hatua muhimu hasa katika kipindi cha miaka 10 tumeshudia wanatanzania wengi wakikata tamaa ndani ya nchi yao nakuhitaji mabadiliko ya kweli.Mh Raisi alitoa ahadi nyingi huku akisisitiza mabadiliko katika uongozi hakika uchaguzi umeisha salama na John Pombe amekuwa Raisi wa Tanzania.Watanzania wengi wanamatumaini makubwa juu yake hasa kutokana na utendaji kazi wake.
Katika hotuba ya kwanza kabisa kama Raisi ameedelea kusisitza kuwa ahadi alizozitoa atazitimiza kwa uhakika na kumuomba mwenyezi amsaidia katika kutimiza yale watanzania wanayotarajia.Hivyo ni kipindi cha utulivu na kila mmoja wetu afanye kazi kwa bidii ili kuweza kusogeza Taifa letu mbele ndio maana kauli mbiu yake ilikuwa HAPA KAZI TU.
0 comments:
Post a Comment