Serikali ya mapinduzi Zanzibar imetoa matamko kuhusu nani anastahili kuongoza serikali katika kipindi hichi cha mpito kuelekea kupata Raisi mpya baada ya Uchaguzi kuhairishwa.Balozi Seifu alisema kutokana na kifungu 28(1)(a)cha katiba kinaweka utaratibu kuhusu muda wa kuendelea kuwa Raisi,na kwamba kwa kufuatana na kifungu hicho mtu mtu aliyechaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ataendelea na dhamana hiyo mpaka pale ambapo Rais anayefuata ale kiapo cha kuwa Rais,na pia kifungu 31 cha katiba kinasema Raisi atashika madaraka hayo baada ya kuapishwa rasmi.
Kutokana na vifungu hivyo Dr Shein ni halali kuongoza Serikali katika kipindi hichi mpaka uchaguzi ufanyike.Wananchi wanaombwa kuwa watulivu na kuendelea na shughuli zao kama kawaida wasirubuniwe na matamshi mengine.Matamko yametolewa na Makamu wa pili wa Rais Balozi Seif Alli Iddi.
0 comments:
Post a Comment