Bi Halima A Bulembo akiwa na umri tu wa miaka 24 ameweza kuapishwa kuwa miongoni mwa Wabunge wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania.Haikuwa rahisi kufika hapo kwani ni takribani zaidi miaka zaidi ya 13 ameanza siasa akiwa darasa tano 2002 akiwa amegombea mara tisa,kushindwa mara tano na kushinda mara tano katika nafasi ya kuwakilisha vijana.Lakini mwaka 2015 ndio amefanikiwa kuwa mbunge wa viti maalumu akiwakilisha vijana,kwa kijana ambaye hana nia na uvumilivu asingeweza kufika alipo Halima leo kwani vijana wengi wanakosa nguvu ya kuwa wavumilivu katika kutimiza ndoto zao wengi wakitamani kupata mafanikio kwa muda mfupi tu.
Halima anamekuwa miongoni mwa mifano ya kuigwa kwa vijana wengi ambayo wanachangamoto nyingi sana katika kutengeneza maisha yao.Kwani ukishindwa kuweka misingi na malengo katika umri huu uwezekano basi uwezekano wa kuwa na maisha bora mbeleni ni mdogo sana.Wito vijana tujiamini na tusimamie malengo yetu hakika tutafika tukiamini katika kujituma zaidi na kuwenga misingi,nia na malengo sahihi.
Halima Bulembo
Akila kiapo cha ubunge
0 comments:
Post a Comment