Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mweshimiwa John Pombe Magufuli hivi karibuni katika kikao chake na Makatibu na Maanaibu Makatibu wakuu na baadhi ya viongozi katika Taasisi kubwa kama Mamlaka ya Mapato na Benki kuu ya Taznania.Mambo mengi yalizungumza hasa lililo nigusa ni hatua yake ya kukata safari zote za nje kwa viongozi mbalimbali wa serikalini.Hii ni hatua nzuri katika kupunguza matumizi makubwa ya serikali.Ni vyema sasa viongozi wetu wajenge tabia ya kufanya kazi na sio kutafuta mianya ya kujiongezea vipato kwa njia halali kama hizi lakini zisizo na tija kwa Taifa kwani viongozi wengi serikalini kwa muda mrefu wamekuwa wakitumia fursa hii zaidi katika manufaa yao binafsi kuliko kwa Taifa kwani tunaishi nao na tunajua hivyo hongera sana Raisi ongeza kasi zaidi katika mambo mengine kama mashangingi,vikao vya ndani visivyo na tija,rasimali za ofisi kama ambazo zimekuwa hazifuati utaratibu mzuri na kuuongezea serikali gharama zisizo za lazima.
Tunaaamini Hapa kazi Tu kwa manufaa ta Taifa letu.
0 comments:
Post a Comment