Tuesday, September 29, 2015

Asernal yafa tena UEFA yapigwa 3-2 na Olympiakos


Matumani ya Asernal kufika hatua ya mtoano yamefifia baada ya kufungwa tena na Olympiakos katika dimba la Emirates.Iliwachukua wageni dakika 33 kupata bao la kwanza kupitia kwa Felipe Pardo kabla ya Theo Walcott kusawazisha dakika ya 35 na dakika ya 40 David Ospina alijifunga mwenyewe.Alexis Sanchez mnamo dakika 65 aliisawazishia tena Asernal lakini kama vile bahati haikuwa kwao tena dakika moja baadae Aflred Finnbogason akahitimisha msiba mwingine na kufunga bao la tatu.Kwa matokeo hayo Asernal wako katika hali mbaya kwani wanaisubilia Bayern Munich ambayo ilipata matokea mazuri kwa kuifunga Dinamo Zagreb 5-0.

1 comments: