Thursday, November 26, 2015

WASOMI WAMWOMBA RAISI MAGUFULI KATIKA UONGOZI WAKE AJALI TAFITI ILI NCHI IPATE MAENDELEO YA KWELI

Wasomi wa Tanzania kwa muda mrefu wameshindwa kuhusishwa kikamili katika kusaidia nchi kupiga hatua kubwa ya maendeleo.Hii inatokana na serikali kwa kipindi kirefu kutochukua hatua ya kujali tafiti mbali mbali ambazo wana taaluma nchini wamekuwa wakizifanya lakini hazifanyiwi kazi na kubaki katika mafaili tu.

Hivyo wanataaluma wamesifia kasi ya magufuli ila wameimuomba kama atakuwa anajali na kufanyia kazi tafiti katika maeneo tofauti zinazofanya na wanataaluma wa kitanzania basi nchi inaweza kupiga hatua kubwa kimaendeleo.Kwani tafiti hizi zitatoa majibu ya matatizo yanayoikabili nchi yetu na zikifuatiliwa kikamilifu maendeleo ya uhakika yatapatikana.Kwani kwa nchi nyingi ambazo zimeweza kuendelea basi tafiti ilikuwa ni chachu ya kufikia maendeleo hayo.Raisi Magufuli chukua ushauri huyo na ufanyie kazi.

Tokeo la picha la images of research and development in africa

0 comments:

Post a Comment