Wednesday, January 20, 2016

Waziri wa Elimu afutilia mbali mfumo wa GPA.

Tokeo la picha la ndalichako

Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia na Mafuzno ya Ufundi ameamua kurejesha mfumo wa zamani wa Madaraja(Divion) badala wa uliokuwa unatumika sasa wa GPA.Hii imekuja baada ya kuwapa NECTA muda wa kupitia mfumo huo sasa na waje na sababu za kisayansi kwani mfumo huo unatumika

Waziri akitoa tamko alieleza baadhi ya mapungufu ya mfumo wa GPA 

1.Mgongano wa mkubwa katika kupanga GPA kuanzia sekondari mpaka vyuo vya ualimu

2.Ufinyu wa uelewa kwa watahiniwa kwani viwango vya kufaulu vimeshuka

3.Wadau hawakuhusishwa katika kuratibu mfumo huyo utumike,hata kamishina wa elimu hajatoa kibali.

Hivyo Prof J Ndalichako ameamua kurudisha mfumo wa zamani wa madaraja.Lakini serikali kupitia wizara hii inahitaji kurekebisha mambo mengi ya msingi katika elimu ambayo imekosa mvuto na kuanza kukosa mvuto.Mambo ni mengi sana ambayo yanapelekea kudorora kwa elimu kubwa ni sera mbovu za mawaziri wanaokalia kiti hiki wengi wanaongoza kisiasa na sio kiataaluma wakati research zinaweza fanyika lakini hamna wa kufuatilia.Hata hivyo mazingira ya elimu kwa upande wa walimu na wanafunzi na vitendea kazi bado nis shida ndio maana kuna hitajika nguvu ya ziada.Kama Waziri ameonyesha nia ya sayansi itumike katika kufanya maamuzi juu ya elimu kunaweza kuwa na tija tuwape muda watimize malengo yao.

0 comments:

Post a Comment