Wednesday, December 2, 2015

RAISI PAUL KAGAME KATIKA PRESHA NA LISTI YA MARAISI WALIOKAA MUDA MREFU

Raisi Paul Kagame wa Rwanda amepitishwa tena kuwania kitu cha uraisi na senata  baadaye 2017 baada ya awamu ya pili kuisha,hivyo atakuwa na uwezo wa kuongoza tena Rwanda kwa awamu ya tatu.Uwamuzi huyo umepigwa vibaya na Marekani kupitia Balozi wake akimwomba Raisi Kagame awe kiongozi bora kwa kuheshimu katiba na kuachia madaraka ifikapo 2017 muda wake utakapoisha.

Tatizo hili limekuwa na mizizi hasa katika bara la Afrika Maraisi wengi wamekuwa wakibadili katiba ili kuweza kupata muda zaidi za kuendelea kuwa Maraisi.Tumeshuhudia nchi nyingi zikiingia kwenye vita  na baadhi ya serikali kupinduliwa kama Sierra Leone.Burundi mapigano yanaendelea huku Raisi Nkurunzinza akijiongezea muda wa kuongoza bila ya kujali maisha ya raia wanakufa na kukimbia nchi yao kila siku.Baadhi ya maraisi waliokaa madarakani muda mrefu ni (1). Teodora Obiang Nguema Mbasogo -Equatorial Guinea Madarakani Miaka 32 (2). Jose Eduardo Dos Santos –  Angola Madarakani miaka 32 (3). Robert Mugabe – Zimbabwe Madarakani Miaka 31 (4). Paul Biya – Cameroon Madarakani  Miaka 29 (5). Yoweri Museveni – Uganda Madarakani Miaka 25 (6). King Mswati III – Swaziland Madarakani Miaka 24 (7). Blaise Compore 24 (8) Kagame 19

Katika kukomesha hili Balozi wa marekani amemwambia Raisi Kagame aaichie madaraka muda ukifika.Na hili lilisitizwa na Barack Obama kuwa hamna haja ya kupenda kuwa Raisi kwani changamoto haziwezi kuondolewa na mtu mmoja alipokuwa akihutubia Umoja wa nchi za Kiafrica -Addis Ababa.Sioni tatizo Maraisi kufanya hivyo hasa Afrika mbona nchi zilizoendelea ni jambo la kawaida na maisha yanaendelea kuimarika kwa wanancghi wao, kinyume na Viongozi wa Afrika cha msingi ni kuweka misingi ya kitaifa iliyoimara na kuweza kuamini mtu fulani ndio kiongozi sahihi kwa mu muda mrefu.


Tokeo la picha la kagame
Raisi Paul Kagame na Mkewe

Raisi wa Burundi Pierre Nkurunziza ambaye amerejea nchini mwake baada ya kushindikana kwa jaribio la mapinduzi ya kijeshi
Raisi Pierre Nkurunzinza.-Burundi.

0 comments:

Post a Comment