Thursday, January 7, 2016

SIMBA YAWAFUNGA WAKUSANYA MAPATO WA UGANDA(URA)

Simba jana usiku iliweka matumaini ya kusonga mbele zaidi katika mashindano ya Mapinduzi yanayofanyika Zanzibar baada ya kuifunga URA bao 1 bila na kukusanya pointi 4 mpaka sasa.

Ibrahim Ajib ndie aliyekuwa shujaa wa jana baada kufunga goli safi katika kipindi cha kwanza.Ajib alipiga shuti la mbali ambalo lilimshinda kipa wa URA.Kipa wa Simba nusura awazawadie URA goli baada ya kushika mpira aliorudidhiwa na kuwapa URA nafasi ambayo walishindwa kuitumia.Mpaka kipindi kinaisha Simba 1 URA 0.

Tokeo la picha la ajib ibrahim

0 comments:

Post a Comment