Sunday, January 17, 2016

ARSENAL BADO BADO SANAAA UBINGWA UINGEREZA

Timu ya Arsenal imeshindwa kujikita kileleni mwa Barclays Premier ligi leo kwa kushindwa kupata pointi zote tatu muhimu katika kipindi hichi baada ya kuambulia sare tasa dhidi ya Stoke City.Kwa matokeo hayo Arsenal licha ya kuongoza ligi kwa tofauti ya magoli dhidi ya leicester City,kama wataendelea kucheza kwa kiwango cha leo basi Ubingwa wa Uingereza utaendelea kuwa historia tena.

Arsenal inakosa kiongozi imara ndani ya timu anayeweza kubadilisha matokeo ndio maana wanaishia kupiga pasi ambazo hazina manufaa na mwisho wanakosa matokeo hari ya wachezaji kutaka ubingwa kwa Arsenal iko mbali sana.Inabidi Wenger atambue vipindi ambavyo timu inahitaji ushindi kitu ambacho kimeo adibu sana kwa arsenal tangu kipindi kile cha kina Thiery Henry,Patrick Viera,Dennis Be,Wiltod,Fred L,Robert P n.k.timu inacheza mechi zote kwa kiwango kile kile.Kwa matokeo hayo Arsena mpaka sasa ina alama 44 nyuma ya Leicester alama 44 na Man City 44.

Arsenal Stoke

0 comments:

Post a Comment