Tuesday, October 13, 2015

ZIMEBAKI SIKU 12:MAGUFULI KUSINI VS LOWASAA KANDA YA ZIWA

Wagombea wa Uraisi wenye mvuto zaidi kwa wananchi Magufuli na Lowassa wanaendelea na mchamchaka wa kutafuta kura kabla ya 25-10-2015 ambapo wananchi wa Tanzania watakapo amua hatma yao ya miaka mitano ya kiongozi nchi yao.Mh Magufuli ameendelea na wimbi la ahadi huko kusini ambapo amesema akichaguliwa kushika nafasi hiyo, atatumia utajiri wa gesi uliopo katika mikoa ya Kusini, kutoa ruzuku kwa vifaa vya ujenzi ili kushusha bei na kuwawezesha wananchi kujenga nyumba bora.Kwa upande wa Mh Lowassa yeye ametaka wananchi wa jiji hilo kujiandaaa na ushindi.Rai kwa watanzania ni kuwa makini katika kujua wanahitaji nini katika kipindi hiki hasa nchi ikiwa inahitaji viongozi wenye uwezo na uthubutu utakao weza kuifanya nchi iwe na uwezo wa kujitegemea zaidi kuliko kusuburi wahisani ambao wamekuwa vigeugeu.Tushikamane kwa maendeleo ya nchi.

0 comments:

Post a Comment