Saturday, October 31, 2015

YANGA YAREJEA KILELENI,HUKU SIMBA IKITOA DOZI TAKATIFU KWA MAJIMAJI

Yanga imefanikiwa kurudi kileleni baada ya kuifunga Kagera Sugar 2-0,Donald Ngoma dakika 23 na Desu Kaseke  dakika 62 wakifunga kila mmoja.

Tokeo la picha la deus kaseke yanga
Ngoma akishangilia na kocha wake

Tokeo la picha la deus kaseke yanga
Deus Kaseke leo amefunga goli lake la kwanza katika ligi.
Simba leo imewapa raha mashabiki wao baada ya kuifunguka Maji Maji idadi kubwa ya magoli 6-1.Alikuwa Ajib alifunga hat-tick dakika ya 8,11 na 42,Hamisi Kiiza alifunga dakika 37 na 80 na Tshabalala dakika 79.Huku Maji Maji ikipata goli kupitia kwa Nchimbi dakika ya 88.

Tokeo la picha la ajib simbaAjib shujaa wa Simba

Tokeo la picha la kiiza simbaDiego(Kiiza)akishangilia goli.

MATAMKO YA MAALIM SEIFU YAKEMEWA ZANZIBAR

Tokeo la picha la images of maalim seifu

Baada ya zoezi la uchaguzi kusitishwa na Tume ya uchaguzi ya Zanznibar.Kwa kipindi sasa kumekuwa na matamko mbali mbali kuelezea sintofahamu hiyo.Balozi za Marekani na Uingereza wakielezea mtizamo wao kuhusu suala la uchaguzi na kutoa matamko kuwa zoezi hilo halina budi kuendelea kwani si haki kwa wananchi wa Zanzibar kwani wanahitaji kupewa haki yao

Kwa upande mwingine baadhi ya viongozi wa Tume wametoa kauli zao kwa kusema kuwa uwamuzi huo wa kusitisha zoezi la kuesabu kura ni uamuzi wa mtu binafsi Mwenyekiti wao Ndugu Jecha na sio wa Tume hivyo wanamtaka afute kauli ili zoezi liendelee

Maalim Seifu mgombea kiti cha Uraisi kupitia CUF ametoa matako mbali mbali tangu kusitishwa kwa zoezi hilo,huku akitaka viongozi wa juu wa serikali ya Zanzibar na Jamuhuri kutoa matako kuhusu hatma ya uchaguzi huo,akieendelea na matamko yako amesema wametoa siku kwa jumuiya ya kimataifa na serikali ikishindikina basi wao wataweza kuamua kama chama nini cha kufanya.

Hata hivyo leo vingoziwa CCM walilani matamko ya Seifu wakisema kuwa yanaweza kuhatarisha amani ya visiwani humo kwa hiyo Ndugu Maalim Seifu hana budi kuachana na matamko ya jinsi hiyo hayo yamezungumza Vuai Nahodha.

Hivyo hakuna budi kwa serikali sasa kutoa tamko kuhusu sakata hili maana mengi yamezungumzwa hivyo kuna haja ya kulimaliza swala hili mapema kabla matatizo makubwa hayatokea. 

CHELSEA YAFA 3-1 DARAJANI,ASERNAL YAIFUNGA 3-0 SWANSEA HUKU MAN CITY IKING'AA NA MANU UNITED YABWANA,MATOKEO HAPA

Mechi ya Chelsea na Liverpool imeisha huku jinamizi likiendelea kuwaumiza Chelsea baada ya kufa 3-1 kwa Liverpool mechi ikiwa Daraji.Magoli yakifungwa na Benteke 1 na Coutihno 2 huku la Chelsea likipatikana dakika 4 kupitia kwa Ramirez.

Philippe Coutinho scores his second goal for Liverpool at Chelsea

Coutinho akifunga goli

Asernal wameza kuwafunga Swansea 3-0 wakiwa ugenini huku Giroud,Campbell na Koscienly  wakifunga kila mmoja.


Olivier Giroud scores Arsenal's first goal against Swansea

Giroud akifunga goli

Man United walishindwa kutamba baada ya kutoka sare la Crystal Palace ya bila kufunguna.

Wayne Rooney (right)

Man City iliendelea kujikita kileleni kwa tofauti ya magoli na Asenal baada ya kuifunga Norwich 2-1.Otamendi na Toure wakifunga magoli ya Man city.

Yaya Toure penalty

Yaya Toure akifunga goli lake kwa penati.


MATOKEO YA LEO

LEADERS HAPATOSHI LEO USIKU WIZKID ANAHAMU YA KUONA MASHABIKI WAKE WA TANZANIA

Wizkid amewasili jana usiku na kutoa ahadi ya kufanya kweli katika onyesho lake la Leaders chini ya udhamini KING SOLOMONI HALL akiojiwa na Sammisago wa EATV alisema mengi kwamba yeye ni mtu mchechi pia,yuko makini katika kuchagua makini ila siku zote anamshukuru Mungu kwa alipofikiwa kwani anajua historia yake.

Kwa wapenzi wa mziki leo sio siku ya kukosa mtu maana jamaa atafanya kweli akipigwa tafu na Daimond,Christian Bella,Fid Q na wengine tukutane Leaders watu wangu.


Wizkid Airport Dar.

Friday, October 30, 2015

MAGUFULI NA SAMIA WAKABIDHIWA VYETI NA KUAHIDI KUWATUMIKIA WANANCHI KWA DHATI

Raisi Mteule baada ya kupokea cheti kutoka kwa Jaji Lubuva

Raisi Mteule amekabidhiwa cheti chake cha kudhibitisha kuwa mshindi baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika 25-10-2015.Raisi huyo mteule amesema atawatumikia wananchi kwani anadeni kubwa na anaona ugumu wa kazi iliyopo mbele yake.
Ameendelea na kuwapa angalizo watendaji wabovu hatawavumilia hata kidogo hivyo watimize majukumu yao kikamilifu la sivyo atafukuzwa tu.Na yeye atakuwa ni Raisi wa nchi nzima hivyo anaomba wananchi wote wamsaidie.
Akiwa na Mgombea wa ACT Anna.


Baadhi ya sehemu ya wanachama waliokuwepo kwenye ukumbi.

WIZKID KUTUA BONGO LEO,JE AMETOKEA WAPI?

Tokeo la picha la IMAGES OF WIZKID

Ayodeji Ibrahim Balogun ambaye anajulikana kama Wizkid ni mwanamuziki,mtunzi kutoka Nigeria ambaye amezaliwa 16-July-1990,Surulere,Lagos State..Wizkid ameenza muziki akiwa kijana wa umri miaka 11.Alitoa Album yake ya kwanza mwaka 2001 akishirikiana na Glorious Five iliyoitwa LIL PRINZ.Mwaka 2009 alisaini  mkataba BANK W'S IMPRINT EMPIRE MATES ENTERTAINMENT.2010-11 ndio mwaka ulimtambulisha Wizkid na wimbo wake HOLLA AT YOUR BOY katika album yake iliyoitwa SUPERSTAR ikiwa na nyimbo kama LOVE MY BABY,PAKURUMO,DON'T DULL na mwaka 2014 alitoa albamu ya pili AYO iliyokuwa na nyimbo kama ONE QUESTION na SHOW YOU THE MONEY.Licha ya kuwa mwimbani wa kujitegemea WIZKID ameshirikiana na wanamuziki wengi sana Bracket,Iyanya,Jesse Jagz,Kcee,R2Bees,Maleek Berry na wengine wengi.Licha ya hayo pia amepata tuzo nyingi BET AWARD,MOBO AWARD,CHANNEL O,THE HEADIES AWARDS,GHANA MUSIC AWARD na nyingine nyingi.Forbes na Channel o's ilimtaja kuwa kati wanamuziki matajiri Africa akishika namba 5 na mwaka 2014 alikuwa mwanamuziki wa kwanza kabisa kuwa na wafuasi zaidi ya millioni moja katika mtandao Wa kijamii wa Twitter.

Kijana anatua leo hii bongo kwa ajili ya SHOW kali hapo kesho katika viwanja vya leaders ikiwa ndio mara yake ya kwanza kufika Tanzania akiwa anatamba na kibao chake cha OJUELEGBA.Hakika kesho Leaders kutawaka kwani kuna wanamuziki kibao wanaofanya vizuri Tanzania watakuwepo kama Diamond na Bella.Viingilio ni 100,000 kwa VIP na 20,000 kawaida.Msikoshe huyo ndio wizkid  kwa ufupi.

Tokeo la picha la images of wizkid

Tokeo la picha la images of wizkid


Thursday, October 29, 2015

DUNIA YAISHUKIA ZEC ZANZIBAR,TANZANIA BARA FUKUTO ILA WASUBIRI SAUTI YA MAGUFULI KAMA RAISI MTEULE KWA MARA YA KWANZA



Tokeo la picha la zanzibar zec
Marekani na Uingereza zimeeleza masikitiko yao juu ya utaratibu uliofanywa na ZEC kusitisha
 mchakato mzima wa uchaguzi Zanzibar.Huku wakitoa matamko ya uchaguzi huo uendelee na hamna sababu ya kuwanyima haki Wanzibari.Mpaka sasa hakuna tamko lolote kutoka serikalini kuhusu mchakato na vuguvugu linaloendelea.Tanzania bara Rais mteule wa awamu ya tano Mh John Magufuli bado hajapata muda wa kuzungumza na wananchi hiyo ndio shauku inayo subiliwa kwa hamu kwani jana mitaa mbali mbali ya Tanzania Bara wananchi walijitokeza wakifurahia ushindi huo.Kweli mambo yameisha Bara,tuombe afanye kama alivyoahidi tuwenze kupata mabadiliko ya kweli na sio mbwembwe za kampeni tu.

Mungu  atuongoze na Tunamuombea Magufuli afanye mabadiliko katika Katiba yetu tuweze kuwa na Tume Huru ya uchaguzi na vingine vingi ambavyo vitampa mwananchi uwezo wakusimamia nchi yake tukumbuke DEMOKRASIA ni nguvu ya wananchi ikiwa kinyume kamwe hamna demokrasia.Ni jambo la msingi na hata wasimamzi kutoka Africa Mashariki wametoa angalizo hili.

Tokeo la picha la images of tanzania ccm supporters

UWIZI WA KURA HAITI WASABABISHA MAAANDAMO

Tokeo la picha la haiti voters images

Wanachi wa Haiti wanaosuburi matokeo baada ya kupiga kura kuchagua viongozi wao wa,Waandamanaji hao walijitokeza mabarabarani baada ya mgombea wanaomuunga mkono Moise Jean-Charles, kudai kuwa kura zake zimeteketezwa moto ama kufichwa.Wanaiishtumu tume ya uchaguzi nchini humo kwa kukiuka kanuni na utendaji wa uchaguzi huru na wa haki.Waangalizi wa umoja wa matafa wamesifu utendaji kazi wa tume hiyo ya uchaguzi wakisema kuwa kwa kiasi kikubwa uchaguzi huo ulikuwa wa haki .Hata hivyo maafisa wamepigwa na butwaa baada ya madai hayo ya kuibiwa kura kuibuka na sasa wameanzisha uchunguzi kutathmini ukweli wake.Matokeo ya kimsingi yanatarajiwa kutangazwa juma lijalo.

Tokeo la picha la haiti voters images


AZAM RAMSI KILELENI YAIPIGA 4-2 JKT RUVU






Azam FC imekaa kileleni mwa Ligi Kuu Bara baada ya kuichapa Ruvu JKT kwa mabao 4-2 kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, leo.


Kwa ushindi huo, Azam FC imefikisha 22 na kukwea kileleni siku ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa awamu ya tano, John Pombe Magufuli kupitia CCM ametangazwa rasmi.

Mabao ya Azam FC yamefungwa na John Bocco aliyefunga mawili, Didier Kavumbagu Na Kipre Tchetche wakati mawili ya JKT yalifungwa na Najim Magulu na Samwel Kamuntu.


Mechi ilikuwa kali, JKT ambayo sasa kocha wake wa muda ni Abdallah Kibadeni ilionyesha soka safi lakini haikuwa makini katika ufungaji.

Achana na hivyo, safu yake ya ulinzi pia iliruhusu washambuliaji wa Azam FC kupenda na kufanikiwa kufunga kiulaini.


Hata hivyo, Azam FC ilionekana kucheza kwa kujiamini zaidi ikipanga mashambulizi kutokea nyuma na kufanikiwa kupata ushindi huo mkubwa na kukaa kileleni mwa ligi kuu ya Tanzania Bara

MAALIM SEIF AMTAKA RAISI KIKWETE KUBEBA DHAMANA ILI KUSIMAMIA SHERIA NA KATIBA YA NCHI

Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Chama hicho Mtendeni Zanzibar. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui Picha: OMKR


Mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Chama hicho Mtendeni Zanzibar. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui. Picha: OMKR
Zanzibar: Mgombea wa Urais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amemuomba Rais Jakaya Kikwete na Rais Ali Mohamed Shein kubeba dhamana ya uongozi katika siku hizi chache zilizobaki za uongozi wao kwa kusimamia katiba na sheria za nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mtendeni Maalim Seif amesema marais hao wawili kuheshimu maamuzi ya Wazanzibari waliyoyafanya tarehe 25 Oktoba na kuwataka washirikiane nae katika kuinusuru Zanzibar.
“Nawaomba sana Rais Kikwete na Rais Shein kukwepa matumizi ya nguvu na badala yake tushirikiane kutunza amani na haki za wananchi. Mimi niko tayari kushirikiana nao kama ambavyo nimekuwa nikifanya mara zote. Tushirikiane kuiepushia Zanzibar na Tanzania fedheha ya kimataifa”. Alisema Maalim Seif.
Akizungumzia kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi iwapo ni halali au sio halali Maalim Seif amesema lile lilikuwa ni tamko binafsi la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) Jecha Salum Jecha ambapo Chama Cha Wananchi (CUF) kimetiwa nguvu na tamko la Makamishna wawili wa Tume waliothibitisha kwamba tamko lile ni lake binafsi.
“Ni kwamba hakukuwa na kikao cha Tume kilichokaa kuamua yaliyosemwa na Jecha, na kwamba hakuna misingi ya kikatiba na kisheria ya tamko lile” alisema Maalim Seif na kuongeza kwamba.
“Jana jopo la wanasheria wa CUF lilikutana kuangalia kwa kina kama kuna misingi ya kikatiba na kisheria ya tamko lile binafsi la Jecha Salim Jecha, na limetoa hoja za msingi zifuatazo kwa kuanzia muundo wa Tume ambapo  Kifungu 119(1) kinaanzisha Tume ya Uchaguzi yenye wajumbe saba (7) akiwemo Mwenyekiti wao.
Alisema (1) Kifungu 119 (10) kinatamka kuwa: “Kiwango cha mikutano ya Tume ya Uchaguzi ni Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wane na kila uamuzi wa Tume ni lazima uungwe mkono na Wajumbe walio wengi”.
Aidha alisema (1) Kwa sababu Tume haikukaa kwa pamoja ikiwa na Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti na angalau wajumbe wengine wanne, na kwa sababu maamuzi yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Tume yalikuwa ni yake peke yake, maamuzi hayo kikatiba ni batili na hayana nguvu zozote.
Maalim Seif ambaye ni Katibu Mkuu wa CUF alisema waangalizi wote wa uchaguzi ikiwa ni pamoja na SADC, AU, Commonwealth Observer Team, European Union Election Observation Team, Waangalizi kutoka Uingereza na Marekani, na TEMCO, wote walisema mbali na dosari ndogo ndogo uchaguzi ulikuwa huru, wa haki na amani.
Aidha aliwaambia waandishi wa habari kwamba Mwenyekiti wa ZEC mwenyewe naye pia alisema uchaguzi ulikuwa huru na wa haki ambapo Mwenyekiti huyo huyo alisimamia kazi ya uhakikiwa matokeo na kutia saini fomu za matokeo yaliyohakikiwa na kuthibitishwa za majimbo 31 ya Unguja na kuyatangaza matokeo hayo kabla.
“Kwa nini ghafla ilipofika siku ya tatu ambayo ni jana aligeuka na kukataa kuendelea na uhakiki na badala yake kudai eti kulikuwa na mambo kadhaa ya kufanya uchaguzi huo usiwe huru na wa haki? Tena dosari zenyewe za tamko lake eti ni pamoja na wajumbe wake kuvua mashati na kutaka kupigana” alisema Maalim.
Akizungumzia suala la baraza la Wawakilishi jipya Maalim Seif alisema Kifungu 92(1) cha Katiba ya Zanzibar kinaeleza kwamba maisha ya Baraza la Wawakilishi ni miaka mitano tokea lilipoitishwa mkutano wake wa mwanzo hivyo Kifungu 90(1) kinaeleza kwamba mkutano wa mwanzo wa Baraza la Wawakilishi utafanyika si zaidi ya siku 90 tokea Baraza lilipovunjwa kwa ajili ya kuitishwa uchaguzi.
Kuna masuali kadhaa ya kujiuliza alisema Maalim Seif ikiwemo ni “Rais yupi ataitisha Baraza?, Wawakilishi wapi wataitwa (wakati hawapo)?, Yote haya yanaleta mgogogro wa kikatiba ambao umesababishwa na mtu mmoja anayeitwa Jecha Salim Jecha kwa sababu tu ya kufuata maelekezo ya chama chake cha CCM”. Alihoji Maalim Seif huku akionekana kuongea kwa kujiamini.
Hata hivyo alisema kuna suali la muundo wa mpito ambapo kama uchaguzi utarejewa, kama anavyotaka Mwenyekiti wa Tume, jambo ambalo alisema halikubaliki kwa sababu ya kukosa misingi ya kikatiba na kisheria, ina maana kuwa serikali itakuwa haipo.
Akitoa sababu za kutokuwepo Maalim Seif alisema kwanza muda wa Urais ni miaka mitano kuanzia tarehe aliyochaguliwa kwa mujibu wa kifungu 28(2) cha Katiba, Ingekuwa tamko la Jecha Salim Jecha ni halali, basi maana yake hakuna Rais anayefuata kwa sababu ya kufutwa kwa uchaguzi, hivyo hakutakuwa na kiapo cha kumuapisha rais mpya. Kwa msingi huo, msharti ya kifungu cha 28(1)(a) hayana nafasi katika mtafaruku huu uliosababishwa na mtu mmoja.
“Hiyo maana yake, kipindi hicho sasa kitakuwa tete na haijulikani kikatiba ni nani ataongoza nchi? Tunasema hivyo kwa sababu vifungu vya Katiba 33(1) na (2) havitumiki hapa kwa suala la kuwa wazi kwa kiti cha Urais na kukaimiwa kwa nafasi hiyo”. Aliongeza.
Alisema hiyo ni kwa sababu nafasi ya Urais haipo kwa sababu itakuwa imemaliza muda wake ifikapo tarehe 2 Novemba, 2015, siku ambayo Urais wa Dk. Ali Mohamed Shein unakamilisha miaka mitano kamili.
Halikadhalika Maalim Seif alitaka kujua jee katika suala hilo suluhisho ni nini? “Kutokana na hoja tulizozieleza hapo juu, ni wazi kwamba tamko la Jecha Salim Jecha ni lake binafsi na kama tulivyotangulia kusema, halina misingi ya kikatiba na kisheria. Kwenye taarifa yake alisema kuwa “… kwa uwezo nilionao …”. Masuala ya kujiuliza ni uwezo upi? Chini ya kifungu kipi cha Katiba au Sheria ya Uchaguzi?” alihoji.
Katika kutilia nguvu hoja yake hiyo ya kisheria Maalim Seif alisema kwa kifupi, ni kwamba Mwenyekiti wa ZEC uwezo huo hana kikatiba na kisheria na kwa msingi huo, maamuzi yake hayo ni batili.
Kufuatilia masuali hayo ambayo majibu yake yapo kisheria Maalim Seif alisema  CUF inasisitiza kile kinachodaiwa na waangalizi wote wa uchaguzi waliotoa taarifa zao kwamba uamuzi wa Mwenyekiti wa ZEC ni uamuzi wake binafsi pekee na haukuwa uamuzi wa Tume, kwani hakukuwa na kikao chochote cha Tume kilichokaa kufikia uamuzi huo.
Alisema uamuzi huo uwekwe upande na Jecha Salim Jecha amepoteza sifa ya uadilifu ambayo ni msingi mkuu wa kazi ya Tume ya Uchaguzi katika kusimamia maamuzi ya Wazanzibari ambao kikatiba (kwa mujibu wa kifungu cha 9(2) (a) ndiyo wenye mamlaka ya kuwaweka madarakani viongozi wa Serikali.
“Hivyo, anapaswa awajibike kwa hatua yake ya kuiingiza nchi katika mgogoro pasina sababu yoyote na ajiuzulu” alisema Maalim Seif huku akionekana na furaha katika mkutano huo wa waandishi wa habari.
Aidha alishauri Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar waendelee na kazi ya kukamilisha uhakiki na majumuisho ya matokeo ya uchaguzi kwa majimbo 14 yaliyobaki na kisha kumtangaza mshindi wa uchaguzi wa Rais wa Zazibar.
Alisema baada ya ukamilishaji huo alisema mshindi wa nafasi ya Urais wa Zanzibar aapishwe, Viongozi wa CUF na CCM washirikiane kuunda Serikali mpya ya Umoja wa Kitaifa itakayoiongoza Zanzibar katika miaka mitano ijayo.
“Kwa maana hiyo, kitumike kifungu 42(6) cha Sheria ya Uchaguzi kinachoeleza kwamba kama kuna matatizo yoyote katika vituo vya kupigia kura a na matokeo hayawezi kutolewa ndani ya siku tatu; basi Tume iendelee kuhesabu na kuhakiki kura na kutangaza matokeo ndani ya siku tatu nyengine na shughuli za kiserikali ziweze kuendelea” aliongeza.
Katika hatua nyengine Malaim Seif alirejea tena kauli yake ya kuhimiza Amani na kuwataka wafuasi wake na wananchama wa CUF na Wazanzibari wote kwa ujumla kuendelea kuwa watulivu na kutunza amani ya nchi yetu huku wakitambua kwamba tutayasimamia maamuzi yao waliyoyafanya tarehe 25 Oktoba, 2015.

MAGUFULI NDANI YA IKULU NA KIKWETE KATIKA SHANGWE



Raisi anayemaliza muda wake akiwa na Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam katika kumpongeza baada kutangazwa kuwa Raisi wa awamu ya tano

MAGUFULI NDIE RAISI AWAMU YA TANO




Tokeo la picha la images of magufuli

RAISI WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

Tume ya Tanzania ya uchaguzi imemtangaza Ndugu John Magufuli kuwa raisi wa awamu ya Tano.Pongezi kwake na Chama Cha Mapinduzi Mungu amjalie awaongoze wananchi vyema.Amefanikiwa kuongoza vyama vyote kwa asilimia 58% ya kura zote za Uraisi zilizopigwa 25 na 26 kwa baadhi ya majimbo.Mungu Ibariki Tanzania tuone mabadiliko tuliyoahidiwa.

Wednesday, October 28, 2015

MAREKANI YATAKA MCHAKATO UCHAGUZI ZENJ UENDELEE,SEIFU ATAKA JUMUIYA KIMATAIFA IINGILIE

Tokeo la picha la embassy of usa in dar es salaam images



Balozi ya Marekani imeomba ZEC iendeleee na mchakato wa kutangaza matokeo ili iwape Wanzanzibari haki yao kwani ni vyema kuheshimu haki yao.Tume ya uchaguzi ilichukua hatua hiyo jana huku ikitoa orodha ya changamato kupelekea kusitisha zoezi zima.Ingawa bado sintofahamu inaendelea kwani Mgombea kupitia CUF Maalim Seif amepinga.Tuombee tu mchakato uendelee na wananchi wapewe haki yao.

SIMBA YAIPIGA COASTAL DAR,YANGA YABANWA NA MWADUI,MTIBWA MBELE KWA MBELE,AZAM LEO,MATOKEO HAPA


Tokeo la picha la IMAGES KIIZA AKISHANGILIA

Simba jana ilirejesha matumaini baada ya kuifunga coasta union katika uwanja wa Taifa bao 1-0 Kiiza akiwa shujaa baadaya majeruhi.

Tokeo la picha la NGOMA DONALD  IMAGES

Yanga ilitoka sare 2-2 na Mwadui huko Shinyanga huku ngoma akipiga zote mbili.

MATOKEO YA JANA

MWADUI 2 YANGA 2
SIMBA 1 COASTAL UNION 0
TOTO AFRICANA 1 MGAMBO JKT 0
MTIBWA SUGAR 1 KAGERA SUGAR 0
MBEYA CITY 1 MAJIMAJI 1
NDANDA 0 STAND UNITED 0

VIGOGO WAENDELEA KUBORONGA CAPITAL ONE,KLOP AONJA USHINDI NA LIVERPOOL,MAN CITY YAUA.


Louis van Gaal


Timu vigogo nchini Uingereza bado wameendelea kuboronga kwenye LEAGUE ONE jana Manchester ilishuhudia ikitolewa katika mikwaju ya penalti dhidi ya Middlesbroug kwa 3-1 huku Wayne Rooney,Ashley Young na Michael Carrick wakikosa penati.

Wayne Rooney
Rooney akirudi baada ya kukosa penati


Liverpool iliyochini ya kocha mpya mjerumani Klop ilipata ushindi wa kwanza dhidi ya Bournemouth kwa kuilaza 1-0,Beki Cylne akiwa shujaa.

Liverpool manager Jurgen Klopp
Klop akishangilia


Manchester City ilifungisha Crystal Palace kwa kuibamiza 5-1,De Bruyne akipiga goli lake la sita dakika 44,mengine Bony 1,Yaya Toure 1,Garcia Alonso 1 na Kelechi Iheanacho 1



Kevin De Bruyne

HATIMAYE MATOKEO ZANZIBAR YAFUTWA


Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Salim Jecha Salim ametangaza kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi visiwani humo akisema uchaguzi huo ulijaa kasoro nyingi.
Kulingana na mwanahabari wa BBC aliyeko hilo Sammy Awami, mwenyekiti huyo ametangaza hatua hiyo kupitia runinga ya serikali visiwani ZBC.
Bw Jecha amesema kuwa uchaguzi huo haukuwa wa haki na kwamba kulikuwa na ukiukaji mkubwa wa sheria za uchaguzi, kwa mujibu wa taarifa ambayo baadaye imetumwa kwa vyombo vya habari.
Amesema baadhi ya makamishna wa tume hiyo, badala ya kutekeleza majukumu yao inavyotakiwa kikatiba "wamekuwa ni wawakilishi wa vyama vyao".
"Kumegundulika kasoro nyingi katika uchaguzi huu miongoni mwa hizo ni kubainika kwa baadhi ya vituo hasa Pemba vimekuwa na kura nyingi kuliko daftari la wapiga kura wa kituo husika."
Amesema hilo ni jambo la kushangaza ikizingatiwa kwamba "baadhi ya wapiga kura hawakwenda kuchukua vitambulisho vyao vya kupigia kura".
Kadhalika, amesema kura hazikupata ulinzi mzuri hususan kisiwani Pemba ambako amesema kuwa baadhi ya mawakala wa baadhi ya vya vyama vya siasa katika kisiwa hicho walifukuzwa.
Ameongezea kuwa vijana katika eneo hilo walivamia vituo vya kupigia kura kwa lengo la kutaka kuzua ghasia, na pia vyama vya siasa vilionekana "kuingilia majukumu ya tume ikiwemo kujitangazia ushindi na kupelekea mashindikizo kwa tume."
Image captionHii ni sehemu ya taarifa ya Bw Jecha
"Nimeridhika kwamba uchaguzi huu haukiwa wa haki na kuna ukiukwaji mkubwa wa sheria na taratibu za uchaguzi," amesema Bw Jecha.
"Hivyo, kwa uwezo nilionao natangaza rasmi kwamba uchaguzi huu na matokeo yake yote yamefutwa na kwamba kuna haja ya kurudia uchaguzi huu."
Tangazo la mwenyekiti huyo limetolewa huku hali ya wasiwasi ikiendelea kutanda visiwani humo.
Siku moja baada ya uchaguzi kufanywa, mgombea wa chama cha upinzani cha Civic United From (CUF) Seif Sharif Hamad alijitangaza kuwa mshindi, hatua iliyokemewa na chama cha CCM ambacho mgombea wake Dkt Ali Mohamed Shein amekuwa rais wa visiwa hivyo muhula unaomalizika.
Tume ya uchaguzi visiwani humo pia ilishutumu hatua ya mgombea huyo. Kabla ya kufutiliwa mbali kwa matokeo ya uchaguzi, tume hiyo ya uchaguzi ilikuwa imetangaza matokeo ya majimbo 31 kati ya majimbo 54 visiwani humo.
Hayo yakijiri Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania inaendelea kutoa matokeo ya uchaguzi wa urais. Kufikia sasa imetoa matokeo ya majimbo 155 kati ya majimbo 264.

LOWASSA APINGA MATOKEO YANAYOTOLEWA NA TUME


Tokeo la picha la images of lowasaa
Mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha CHADEMA Edward Lowassa amesema kuwa hatokubali matokeo ya uchaguzi wa urais yanayoendelea kutolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania (NEC).
Kiongozi huyo amesema kuwa ana ushahidi wa kutosha kwamba kuna udanganyifu uliofanyika.
Amesema kuwa kura za chama hicho zimepunguzwa katika vituo vingi vya kupigia kura.
Akihutubia wanahabari pamoja na viongozi wengine wa upinzani, amesema kwamba kura zilizohesabiwa katika maeneo tofauti haziambatani na matokeo yaliyotolewa.
Lowassa ameongezea kwamba maeneo yote ambayo walipata ushindi yamecheleweshwa. Aidha, amelalamikia kukamatwa kwa maajenti wa chama hicho akidai kuwa ni ishara za kutaka kuiba kura.