Marekani na Uingereza zimeeleza masikitiko yao juu ya utaratibu uliofanywa na ZEC kusitisha
mchakato mzima wa uchaguzi Zanzibar.Huku wakitoa matamko ya uchaguzi huo uendelee na hamna sababu ya kuwanyima haki Wanzibari.Mpaka sasa hakuna tamko lolote kutoka serikalini kuhusu mchakato na vuguvugu linaloendelea.Tanzania bara Rais mteule wa awamu ya tano Mh John Magufuli bado hajapata muda wa kuzungumza na wananchi hiyo ndio shauku inayo subiliwa kwa hamu kwani jana mitaa mbali mbali ya Tanzania Bara wananchi walijitokeza wakifurahia ushindi huo.Kweli mambo yameisha Bara,tuombe afanye kama alivyoahidi tuwenze kupata mabadiliko ya kweli na sio mbwembwe za kampeni tu.
Mungu atuongoze na Tunamuombea Magufuli afanye mabadiliko katika Katiba yetu tuweze kuwa na Tume Huru ya uchaguzi na vingine vingi ambavyo vitampa mwananchi uwezo wakusimamia nchi yake tukumbuke DEMOKRASIA ni nguvu ya wananchi ikiwa kinyume kamwe hamna demokrasia.Ni jambo la msingi na hata wasimamzi kutoka Africa Mashariki wametoa angalizo hili.
0 comments:
Post a Comment