Mgombea Uraisi kupitia vyama UKAWA ndugu Edward Lowassa kwa dakika takribani thelathini katika hotuba ya kufunga kampeni alianza kwa kuwashukuru watanzania kwa kipindi chote cha kampeni na kubainisha amejifunza mengi katika kipindi chote alichokuwa akizunguka kutangaza sera za CHADEMA chini ya UKAWA. Na kuahidi kuwa wataiongoza Tanzania katika safari ya uhakika na sio ya matumaini hivyo chama chake kimejizatiti kuwatumikia Watanzania wote;katika kupinga RUSHWA NA UFISADI,KUONGEZA AJIRA,KUTUMIA RASILIMALI KWA MANUFAA YA TAIFA,WATAJENGA BARABARA,WATABORESHA BANDARI,KUDUMISHA ELIMU,HUDUMA BORA ZA AFYA,HUDUMA YA MAJI.Alieendelea pia kutoa mifano ya baadhi ya nchi ambazo zilikuwa kama sisi lakini leo hii ziko mbali mfano wa Korea na Malaysia.Miaka 50 imeoneka bado nchi yetu ni tegemezi na maskini lakini yeye ameahidi kufanyia kazi na kuongoza nchi ifikie kwenye maendeleo huku akitoa sifa kemkem za Raisi bora mwenye kuwajibika kwa dhati,mwenye nidhamu,itikadi sahihi na maadili,pia awe na dira,wajibu wa kuongoza.Hivyo imefika wakati wa mabadiliko kwani CCM imeishiwa pumzi .MWISHO ALIWAASA NA KUOMBA APIGIWE KURA KWANI ATAWEZA KUTII KIU YA WANANCHI KWANI NI UONGOZI SI DHARULA NA YEYE ATAWAWATUMIKIA WANANCHI KWA NGUVU ZOTE NA MUNGU ATAMUONGOZA KWANI YEYE NI MCHA MUNGU.
0 comments:
Post a Comment