Wanachi wa Haiti wanaosuburi matokeo baada ya kupiga kura kuchagua viongozi wao wa,Waandamanaji hao walijitokeza mabarabarani baada ya mgombea wanaomuunga mkono Moise Jean-Charles, kudai kuwa kura zake zimeteketezwa moto ama kufichwa.Wanaiishtumu tume ya uchaguzi nchini humo kwa kukiuka kanuni na utendaji wa uchaguzi huru na wa haki.Waangalizi wa umoja wa matafa wamesifu utendaji kazi wa tume hiyo ya uchaguzi wakisema kuwa kwa kiasi kikubwa uchaguzi huo ulikuwa wa haki .Hata hivyo maafisa wamepigwa na butwaa baada ya madai hayo ya kuibiwa kura kuibuka na sasa wameanzisha uchunguzi kutathmini ukweli wake.Matokeo ya kimsingi yanatarajiwa kutangazwa juma lijalo.
0 comments:
Post a Comment