Azam FC imekaa kileleni mwa Ligi Kuu Bara baada ya kuichapa Ruvu JKT kwa mabao 4-2 kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, leo.
Kwa ushindi huo, Azam FC imefikisha 22 na kukwea kileleni siku ambayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa awamu ya tano, John Pombe Magufuli kupitia CCM ametangazwa rasmi.
Mabao ya Azam FC yamefungwa na John Bocco aliyefunga mawili, Didier Kavumbagu Na Kipre Tchetche wakati mawili ya JKT yalifungwa na Najim Magulu na Samwel Kamuntu.
Mechi ilikuwa kali, JKT ambayo sasa kocha wake wa muda ni Abdallah Kibadeni ilionyesha soka safi lakini haikuwa makini katika ufungaji.
Achana na hivyo, safu yake ya ulinzi pia iliruhusu washambuliaji wa Azam FC kupenda na kufanikiwa kufunga kiulaini.
Hata hivyo, Azam FC ilionekana kucheza kwa kujiamini zaidi ikipanga mashambulizi kutokea nyuma na kufanikiwa kupata ushindi huo mkubwa na kukaa kileleni mwa ligi kuu ya Tanzania Bara
0 comments:
Post a Comment