Saturday, October 24, 2015

MAGUFULI APAGAWAISHA MWANZA(CCM KIRUMBA) KATIKA KUFUNGA KAMPENI ATOA VIPAO MBELE VINGI.




Tokeo la picha la images of magufuli campaign


Ameanza kwa kuwashukuru WANANCHI wote na  mwenyezi Mungu kumfanikishia yote hadi kuifikia  katika kampeni za mwisho.Amevishukuru vyombo vyote vya habari na pia  kukubali ushauri wote aliopewa na wananchi kwa njia ya simu,mitandao vijana na mabango.Pia amewashukuru wagombea wenzake :maswala muhimu aliyoyapa kipaumbele.

  • Swala la maji atalimaliza hasa kuongeza mpaka 85% kwa vijijini na 90% mjini
  • Umeme utakuwa wa uhakika na itakuwa historia kwani gesi itaweza kupunguza shida hii
  • Usalama na Ulinzi atadumisha maslahi na maisha yao kwani yeye ni  Amiri jeshi 
  • Muungano utasimamiwa kwa nguvu zote na atakula sahani moja na yoyote atakaye uchezea
  • Viwanda vyote atavifufua kama vya nguo,ngozi na watu waliovichukua baada ya kubinafsishwa wafanye kazi kweli. 
  • Kilimo cha aina vyote atavidumisha
  • Vijana wote anawashukuru na atawafanyia kazi kufikia mabadiliko
  • Atakuza biashara kwani yeye ni rafiki wao,hasa wawekezaji wakubwa waje kuja kuwekeza katika nchi yetu pia wakati na wadogo
  • Kuongeza ajira nchini kwa kiwango kizuri kabisa.
  • Kuwapa mitaji vijana kuweza kuanzisha makampuni yao
  • Kupunguza ushuru na kuondoa viushuru vyote ambavyo hayana tija hasa kwa watu wenye vipato vya chini
  • Kero za wafanyakazi hasa makato katika mishahara hasa Tume itakapo leta mapendekezo yatafanyiwa kwa haraka sana.
  • Amezungumzia maswala ya utalii iwe sekta itakayokuza uchumi nchini hasa kuongeza watalii mpaka milioni 2  kwa mwaka.
  • Suala la madini hasa wachimbaji wadogowadogo atalishungulikia.
  • Mawasiliano yatadumishwa.
  • Kupunguza bei vifaa vya ujenzi ili kuwawezesha wananchi kupata nyumba bora kwa gharama nafuu.
  • Suala la elimu  limelalamikiwa sana ktk ziara za kampeni  ntalifanyia kazi na watasoma bure mpaka kidato cha nne  na atashughulika na mikopo kwenye vyuo.
  • Afya pia ataboresha kwa kujenga hospitali kuwe na Zahati katika kila kijiji  pia kila Mkoa  uwe na hospitali ya rufaa pamoja na watumishi na madawa ya kutosha. 
  • Miundo mbinu: barabara zitajengwa zaidi
  • Bandari zitaiimarishwa,reli zitajengwa kwa kiwango cha  standard gauge,viwanja vya ndege pia vitaboreshwa.
  • Mahusiano na nchi jirani zetu yatadumishwa zaidi.
Pia ameomba ridhaa ya wananchi wampe kura za ndio ili aweze kutekeleza yale ambayo ameyahidi katika kipindi chote cha kampeni.


0 comments:

Post a Comment