Leo ni siku ya tatu bado headlines za Matokeo ya Uchaguzi Mkuu zimeendelea kutawala vichwa vya habari, ni headlines za Siasa zinazoendelea kutawala kwa sasa Tanzania.
Uchaguzi uliofanyika October 25 2015 ilikuwa ni sehemu ya Watanzania kufanya maamuzi ya Madiwani, Wabunge na Rais atakayeongoza nafasi hizo kubwa tatu kwa kipindi cha miaka mingine mitano, wapo waliofanikiwa kupita, wapo walioshindwa na wapo ambao bado matokeo hayajatoka kwa sababu mbalimbali.
Leo ninayo idadi iliyonifikia ya baadhi ya viongozi waliowahi kuwa kwenye nafasi mbalimbali ikiwemo Wabunge na Mawaziri ambao wameshindwa kupita kwenye uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2015 kwa hiyo hawatoonekana Bunge lijalo.
Dk. Fenela Mukangara– alikuwa Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Godfrey Zambi– alikuwa Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika
Dk. Cyril Chami – Waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara
Dr. Didas Masaburi – aliyekuwa Meya wa Jiji Dar es Salaam
Jerry Silaa – aliyekuwa Meya wa Ilala Dar es Salaam
Christopher Ole Sendeka – aliyekuwa Mbunge wa Simanjiro
Abbas Mtemvu – aliyekuwa Mbunge wa Temeke Dar es Salaam
Murtaza Mangungu – aliyekuwa Mbunge wa Kilwa Kaskazini
Augustino Mrema – aliyekuwa Mbunge wa Vunjo (Kilimanjaro)
Prof. Juma Kapuya – aliwahi kuwa Waziri wa Kazi
Steven Wasira – alikuwa Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
Dk. Steven Kebwe – alikuwa Naibu Waziri wa Afya
Christopher Chiza – alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Uwekezaji na Uwezeshaji
Anne Kilango Malecela – alikuwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Omar Nundu – aliwahi kuwa Waziri wa Uchukuzi
Idd Azzan – alikuwa Mbunge wa Kinondoni Dar es Salaam
Wako Wabunge ambao Majimbo yao bado kuna utata wa matokeo, wengine zoezi la Uchaguzi na kuhesabu Kura ilibidi lirudiwe kutokana na changamoto mbalimbalki zilizojitokeza.
0 comments:
Post a Comment