Wednesday, December 9, 2015

RAISI MAGUFULI AUNGURUMA FELI NA KIKWETE MSOGA ASEMA HAJACHOMEKA KITU


Raisi Magufuli na Mama Janet hapa kazi tuu.

Desemba 9 2015 siku ya uhuru wa Tanzania kwa mara ya kwanza ilisherekewa kwa aina ya pekee badala ya kuwa na sherehe kama ilivyokuwa miaka mingine.Kwa maelekezo na mamlaka ya Raisi ilikuwa ni siku ya usafi nchi yote.

Hata hivyo baada ya usafi Raisi Magufuli alipata wasaa wa kuongea na wavivu pale feli nakutoa yafuatayo.

1.Wavivu wote waunde umoja wao na sio umoja kivuli ili msaada utakao toka serikalini uwasaidie wao ili kuepuka kupata viongozi vibaraka.

2.Kuondoa tozo na sheria ambazo hazina tija kama Fire extinguisher  na kusema maji yenyewe yanaweza tumika kama fire extinguisher 

3.Kuwaomba wavivu kutovua kwa njia haramu kwa kutumia baruti n.k

4.Kuwashukuru watanzania wote kwa muitikio wa zoezi la usafi na kusema hapa kazi tuu.


Kwengine Raisi mstaafu JK baada ya usafi alitoa hotuba fupi akisema yafuatayo

1.Katika uongozi wake alikweza kuongeza mapato mpaka bilioni 900

2.Kupambana na wakwepa kodi ingawa sio kazi la rahisi kwani wakwepa kodi hawataacha ndio maana mapambano yataendelea

3.Alisema wanaomshambulia wanapoteza muda wachonge tuu ni siasa za maji taka hata familia yake hakuusika na hivyo wanaosema hachomoki wanapoteza muda bure kwani kachomeka nini?

4.Wamwache Magufuli afanye kazi yake.

0 comments:

Post a Comment