Monday, November 23, 2015

PAPA FRANCIS KUANZA ZIARA YA KITUME BARANI AFRIKA

Kiongozi  Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani anatarajia kuanza ziara yake barani 
Afrika kwa kudhuru Kenya.Papa Francis anatawasili Kenya siku ya Jumatano tayari kuanza kwa ziara hiyo Barani Afrika ambako atakuwa kwa siku mbili na baadaye kwenda Uganda ambako nako atakuwa kwa siku mbili hadi Novemba 29 atakapoondoka kuelekea Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Eneo la Afrika Mashariki ni eneo lenye wakatoliki wengi na katika miaka ya hivi karibuni waumini hao wamekuwa wakijadili kuhusu kile kinachoonekana kama ni mabadiliko katika sera za kikonsevativu za Kanisa Katoliki.
Papa Francis amekuwa kiongozi tofauti sana na Mapapa waliomtangulia huku akiwa na misimamo tofauti juu ya mambo mbali mbali yanayosimamiwa na kanisa katoliki mfano talaka(mchakato wake),mahusiano ya mapenzi baina ya jinsia zinazofanana.Lakini ni Papa ambaye ameweza kuwa na mvuto mkubwa kwa muda mfupi.Tumuombe ziara yake iwe na mafanikio hasa katika kuimarisha IMANI ya wauumini wa dhehebu hilo.
Tokeo la picha la papa francis
Papa Francis 

0 comments:

Post a Comment