Monday, November 9, 2015

HAPA KAZI TU :MAGUFULI AFANYA TENA ZIARA YA GHAFLA MUHIMBILI

Raisi wa Tanzania ameendelea kutembelea Tasisi za serikali bila kutoa taarifa na jana alipata wa saa wa kutembelea hospitali ya Muhimbili na kujionea mambo yanavyokwenda.Katika ziara hiyo mambo kadhaa ya aibu na yakusikitisha baada ya kukutana na wagonjwa wanao subiri huduma wakiwa wamelala chini huku wakisubili huduma bila ya mafanikio kwa zaidi ya miezi huku viongozi wa hospitali wakitoa taarifa kuwa vifaa vya kutolea huduma za mionzi vikiwa hoi taabani.Raisi katika ziara hiyo alitoa agizo la bodi ya hospitali hiyo kuvunjwa mara moja na Kaimu Mkurugenzi kusimamishwa.

Katika hatua nyingine ambazo serikali imechukua ni kutoa wiki moja kwa marekebisho ya matatizo yote likiwepo ukarabati wa vifaa  muhimu viwe katika hali nzuri,pia serikali imetoa billion 3 kwa ajili ya kulipa madeni na kurebisha matatizo yalionekana na Mweshimiwa Raisi.


0 comments:

Post a Comment