Saturday, November 14, 2015

TAIFA STARS YAWATIA SIMANZI WATANZANIA

Licha ya kucheza soka safi la kufutia mbele ya Algeria timu ya Taifa Stars jana ilishindwa kupata matokeo mazuri.Watanzania walijitokeza kwa wingi licha ya kuwa na vipindi vya mvua kwa siku ya jana ili kuwapa hamasa wachezaji lakini tunaweza sema bahati au uzembe uliofanywa na mabeki wetu na kuruhusu magoli mawili ya harakaharaka kulileta hali ya uhuzuni kubwa ndani ya uwanja wa Taifa hakuna aliye aamini kilichotokea mpaka pale mwamuzi wa kati alipopiga filimbi ya mwisho katika dk 93+ kuashilishia mchezo umekwisha.

Mechi ya jana ilianza saa kumi na nusu ila mwamuzi alibidi kusubili kwa takribani dakika 10 kumi hivi baada ya matukio kabla ya mechi kuanza kumalizika mapema.Alikuwa Eliasi Maguli dk 43 aliweza kuamsha furaha ya watanzani kwa kupiga goli safi kipindi cha kwanza kabal ya Mbwana Samatta dk 54 kufunga la pili katika kipindi cha pili na baada Algeria walisawazisha magoli katika dk 71 kupitia Sliman  katika kipindi cha pili sifa ziende kwa kipa wa Algeria Raisi aliweza kuokoa magoli ya wazi jana.

Taifa Stars sasa wanakabiliwa na mtihani mgumu katika mechi ya marudiano nchini Algeria kwani wanahitaji matokeo sina wasiwasi na timu ya Taifa kama waliweza kucheza katika kiwango kile wanaweza kupata matokeo huko Algeria mpira wa sasa ni dakika tisini na sio historia ni kumpa Koch muda wa kuondoa makosa yaliyojitokeza jana na sio kumtupia lawama kama baadhi ya watu wakisema wachezaji waliobadilishwa hawakupaswa kutolewa hayo ni matokeo ya mpira tuungane kwa maendeleo ya timu yatu.

Tokeo la picha la images of algeria tgeamTimu ya Algeria

Tokeo la picha la images if taifa star
Taifa Stras

0 comments:

Post a Comment