Monday, November 2, 2015

TAIFA STARS YAANZA SAFARI YA KUIVAA ALGERIA SOUTH AFRICA


Timu yetu ya Taifa Stars iko South Africa kwenye kambi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Algeria hapo 14-11-2015 kwenye uwanja wa Taifa.

Wachezaji waliopo Afrika Kusini ni Ally Mustafa, Aishi Manula, Said Mohamed, Juma Abdul, Shomari Kapombe, Ramadhan Kessy, Mohamed Hussein, Haji Mwinyi, Hassan Isihaka, Salim Mbonde, Kelvin Yondani na Nadir Haroub.
Wengine ni Mudathir Yahya, Frank Domayo, Himid Mao, Salum Abubakar, Farid Mussa, Saimon Msuva, Salum Telela, Jonas Mkude, Said Ndemla, Ibrahim Hajibu, Malimi Busungu na John Bocco.
Mshambuliaji wa Stand United, Elias Maguri anatarajiwa kuungana na kikosi hicho kesho baada ya kuitumikia timu yake katika  mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom leo jumatatu dhidi ya Mgambo Shooting katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.
Aidha washambuliaji Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na Mrisho Ngasa wanaocheza soka nje ya nchi, wataungana na wenzao baada ya michezo ya mwishoni mwa wikiendi hii.
Kwa watanzani ni kuwaombea na kuwa na fikra chanya juu ya timu yetu kwa maandalizi ya mechi hiyo dhidi ya Timu bora kabisa barani Afrika hakuna kisichowezekana wao wamefika hapo kwa juhudi nasi ni kipindi cha kusapoti timu yetu na tume iliyoundwa kwa ajili ya kuifanya Taifa Stars iwe bora katika mechi zake za kimataifa.
Tokeo la picha la images of Taifa staRS SOUTH

0 comments:

Post a Comment