Tuesday, November 17, 2015

TAIFA STARS AIBU TUPU ALGERIA YAFUNGWA 7-0 SAFARI NYINGINE 2022.

Timu ya Taifa stars ikicheza soka bovu kabisa ilikubali kipigo cha aibu baada ya kufungwa magoli saba(7).Hali ilionekana kuwa mbaya tangu dakika za mwanzoni kwani wachezaji wa Taifa Stars hakuwa watulivu kama walivyocheza mechi ya kwanza.Hivyo kuwafanya Algeria kutumia nafasi ya kufunga magoli mengi na kufanya Taifa Stars kufungasha kwa jumla ya goli 9 kwa 2.

Ilichukua dakika moja tu kwa Algeria kupata goli kupitia kwa Yacine Brahim ,baadaye F.Ghoulam dk 26,dk 43 Riyad,dk 49,dk 59 F.Ghoulam,dk I.Slimani72 Carl Medjani na 75 I.Slimani.

Katika mchezo huo kiungo Mudhathiri Yahya alionyesha kadi nyekundu baada ya kucheza rafu ya pili.Kwa ujumla taifa Stars walizidiwa kwa kila kitu huku Samatta akionyesha uhai kidogo.Kwa matokeo hayo safari ya Tanzania imeishia hapo mpaka 2022.

0 comments:

Post a Comment