Thursday, November 12, 2015

RAISI MSTAAFU JAKAYA KIKWETE AKABIDHI RASMI OFISI NA KUSIFIA KASI YA RAISI MAGUFULI



Jana katika ikulu ilikuwa siku rasmi kwa Raisi wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete kukabidhi ofisi kwa raisi wa tano Mh Dkt John Pombe Magufuli.

Raisi mstaafu alitoa yake ya moyoni katika makabidhiano hayo kwa kusifia mwanzo mzuri wa safari ya miaka mitano ndani ya ikulu ya Tanzania kuwa inapaswa aendelee nayo pia alisifia juhudi aliyofanya katika kuleta mabadiliko chanya katika hospitali yetu ya Muhimbili pia Raisi mstaafu alikabidhi taarifa yenye kurasa 53 kuelezea nin kimefanyika,nini bado na nini kifanyike.

Raisi wa awamu ya Tano alipongeza serikali iliyopita na kuaahidi kuendelea kuchota hekima zao zaidi kama njia ya kuipeleka Tanzania mbele.


Raisi magufuli akikabidhiwa ripoti na Raisi mstaafu Jakaya Kikwete


0 comments:

Post a Comment