Tuesday, October 13, 2015

CCM KU NANI!!MWAPACHU NAE AACHIA NGAZI

Juma Volter Mwapachu ni Mtanzania amezaliwa 27-09-1942 jijini Mwanza,ni msomi wa sheria katika chuo kikuu cha Dar es Salaam (Mlimani) mwaka 1969.Amewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika serikali ya Tanzania ikiwemo Balozi wa Tanzania nchini India,Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Reli Tanzania na nyingine nyingi tuu,huku akishika wadhifa wa katibu Mkuu wa Umoja wa nchi za Africa Mshariki.Kwa ufupi ni kati ya Watanzania wachache wanoweza kujisifia kwa mafanikio ya kuifahamu serikali yetu kwa takribani miaka 45 si haba.Jambo ambalo linalotia shaka ni uwamuzi wake wa kujitoa CCM huku akiamini kuwa wakati wa MABADILIKO UMEWADIA sasa sisi wananchi tunajiuliza kuna nini ndani ya CCM kwa nini mwaka huu wengi wa wanachama wanakimbia mfano ni Mzee wetu Kingunge bila shaka kuna mambo ya kujifunza hapa kama sio hivyo labda wao wanaajenda zao binafsi.Cha msingi hapa wote wanasema wanahitaji mabadiliko na hiki ndio kiu cha Watanzania wengi hivyo ni jukumu letu kujua tunahitaji nini hapo 25-10-2015.Mungu ibariki Tanzania

0 comments:

Post a Comment