Monday, October 19, 2015

TFF YAFANYA KWELI KWA TAIFA STARS

Hatua ya TFF kuvalia njuga timu yetu ya Taifa ni jambo la kutia faraja wapo watakao sema wamechelewa ila naamini kwa nia hii na ikiwa endelevu basi siku moja kile tunachokihitaji kama taifa katika ulimwengu wa soka tutafika.Niliwahi kusikia mmoja wa rafiki yangu akisema Rais(Malizi) wa TFF anaipenda sana Taifa Stars hii imedhihirisha wazi Watanzania ni wakati wa kuijali,kuipenda na kuisapoti timu yetu ya Taifa.

TFF katika kufanikisha hili imekuja na kauli mbiu hii  “NCHI YETU, TIMU YETU, TAIFA LETU, USHINDI WETU na kuunda kamati itakayo hakikisha Timu yetu inafika mbali.Kamati hiyo inaundwa na Mwenyekiti Farough Baghozah,Michael Wambura-Makamu Mwenyekitina na Bi Teddy Mapunda-Katibu.Jopo hili linaongoza kamati nne(4)
 1. Maandalizi ya timu, zikiwemo huduma kwa timu ya Taifa stars
 Mwenyekiti–Imani Madega
 Wajumbe–Msafiri Mgoyi,Teddy Mapunda.
2. Uhamasishaji wa mchezo (Michezo ijayo) na Masoko
 Mwenyekiti–Juma Pinto
 Wajumbe–Baraka Kizuguto, Mlamu Ng’ambi, Charles Hamka, Hashim  Lundenga, Maulid Kitenge, Shaffih Dauda, Salehe Ally, Peter Simon,  Edo Kumwembe na Mahmoud Zubeiry.
 3. Kamati ya Fedha
Mwenyekiti–Farough Baghozah
Wajumbe–Teddy Mapunda, Michael Wambura, Imani Madega, Juma Pinto, Isaac Chanji, Moses Katabaro na Edgar Masoud.
4. Mikakati ya ushindi 
Iitakuwa na kamati ndogondogo na zitakuwa na wajumbe mbalimbali wakiwemo Mwenyekiti Farough Baghozah, Teddy Mapunda, Mohamed Nassoro, Philemon Ntahilaja, Isaac Kasanga, Cresencius Magori.


0 comments:

Post a Comment