Monday, October 19, 2015

WATANZANIA WAHESABU SIKU TANO KABLA YA KUVUNA KILE WATAKACHO KIPANDA 25-OCT-2015

Hakika tulikuwa tunahesabu miaka,miezi,wiki na leo siku kabla ya Watanzania kuamua ni mabadiliko yapi wanayoyahitaji.Mengi yamepitwa na wagombea wetu wa nafasi mbalimbali wamesema mengi na kuaahidi nini watatufanyia kama tutawapa zamana ya katika nafasi walizo omba ili kuweza kuleta mabadiliko.Tunaweza chukulia kama jambo la kupita ila litaamua mambo yetu mengi ndani ya miaka mitano ijayo.Kwa hivyo hatuna budi kufanya upembuzi wa kina na kuwapa watu ambao wanania katika kuendeleza Taifa letu lenye matatizo lukuku kama ya rushwa,umaskini,miundo mbinu mibovu n.k.Hakika tukipanda vizuri tutavuna vizuri na kinyume chake tukipanda vibaya tutavuna vibaya,tusifanye makosa twende tukiwa na akili timamu tusiziache nyumbani na tufanye maamuzi sahihi.Mungu ibariki Tanzania 


0 comments:

Post a Comment