Friday, October 30, 2015

WIZKID KUTUA BONGO LEO,JE AMETOKEA WAPI?

Tokeo la picha la IMAGES OF WIZKID

Ayodeji Ibrahim Balogun ambaye anajulikana kama Wizkid ni mwanamuziki,mtunzi kutoka Nigeria ambaye amezaliwa 16-July-1990,Surulere,Lagos State..Wizkid ameenza muziki akiwa kijana wa umri miaka 11.Alitoa Album yake ya kwanza mwaka 2001 akishirikiana na Glorious Five iliyoitwa LIL PRINZ.Mwaka 2009 alisaini  mkataba BANK W'S IMPRINT EMPIRE MATES ENTERTAINMENT.2010-11 ndio mwaka ulimtambulisha Wizkid na wimbo wake HOLLA AT YOUR BOY katika album yake iliyoitwa SUPERSTAR ikiwa na nyimbo kama LOVE MY BABY,PAKURUMO,DON'T DULL na mwaka 2014 alitoa albamu ya pili AYO iliyokuwa na nyimbo kama ONE QUESTION na SHOW YOU THE MONEY.Licha ya kuwa mwimbani wa kujitegemea WIZKID ameshirikiana na wanamuziki wengi sana Bracket,Iyanya,Jesse Jagz,Kcee,R2Bees,Maleek Berry na wengine wengi.Licha ya hayo pia amepata tuzo nyingi BET AWARD,MOBO AWARD,CHANNEL O,THE HEADIES AWARDS,GHANA MUSIC AWARD na nyingine nyingi.Forbes na Channel o's ilimtaja kuwa kati wanamuziki matajiri Africa akishika namba 5 na mwaka 2014 alikuwa mwanamuziki wa kwanza kabisa kuwa na wafuasi zaidi ya millioni moja katika mtandao Wa kijamii wa Twitter.

Kijana anatua leo hii bongo kwa ajili ya SHOW kali hapo kesho katika viwanja vya leaders ikiwa ndio mara yake ya kwanza kufika Tanzania akiwa anatamba na kibao chake cha OJUELEGBA.Hakika kesho Leaders kutawaka kwani kuna wanamuziki kibao wanaofanya vizuri Tanzania watakuwepo kama Diamond na Bella.Viingilio ni 100,000 kwa VIP na 20,000 kawaida.Msikoshe huyo ndio wizkid  kwa ufupi.

Tokeo la picha la images of wizkid

Tokeo la picha la images of wizkid


0 comments:

Post a Comment