Saturday, October 24, 2015

LEO NI SIKU YA UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA-TUIMBE SOTE


Tokeo la picha la flag of tanzania



Wimbo huu unachochea UPENDO  na kudumisha UZALENDO wa WATANZANIA na nchi yao,hivyo basi ni vyema TUPIGE KURA zetu kwa AMANI huku tukikumbuka TANZANIA ni yetu SOTE.

Lyrics: 

Chorus: (1x) 
Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote, 
Nchi yangu Tanzania jina lako ni tamu sana, 
Nilalapo nakuota wewe, 
Niamkapo ni heri mama we! 
Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote. 

1. Tanzania Tanzania ninapokwenda safarini kutazama maajabu, 
Biashara nayo makazi, 
Sitaweza kusahau mimi mambo mema, 
Ya kwetu kabisa, 
Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote. 

Chorus (1x) 

2. Tanzania Tanzania watu wako ni wema sana, 
Nchi nyingi zakuota nuru yako hukana tena, 
Nawageni wakukimbilia ngome yako imara kwelii we, 
Taniania Tanzania heri yako kwa mataifa. 

Chorus (1x) 

3. Nchi nzuri Tanzania karibu wasio kwao, 
Wenye shida na taabu hukimbizwa na walowezi, 
Tanzania yawakaribisha mpigane kiume chema we, 
Tanzania Tanzania mola awe nawe daima. 

Chorus (1x)

0 comments:

Post a Comment